MMOMONYOKO WA MAADILI WATAJWA KUWA CHANZO CHA RUSHWA YA NGONO VYUONI.

 


📌HAMIDA RAMADHANI

PAMOJA na Serikali kuchukua hatua kadhaa za kupambana na rushwa, ikiwemo rushwa ya ngono lakini bado kumekuwepo na malalamiko ya kukithiri kwa rushwa ya ngono nchini na kilio kikubwa ikiwa ni mmomonyoko wa maadili.

Akiongea katika kikao kazi cha Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) na waandishi wa habari katika  kutoa ufafanuzi wa utafiti wa rushwa ya ngono uliofanywa na Taasisi hiyo Afisa Takukuru Jiwenary John amesema zipo sababu nyingi zinazosababisha kuendelea kuwepo kwa vitendo vya rushwa ya ngono.

Amesema Katika utafiti uliofanywa katika Taasisi za elimu ya juu vyuo vikuu viwili Chuo Kikuu cha Dar Es salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) sababu zinazosababisha ni pamoja na Mmomonyoko wa maadili,matumizi mabaya ya madalaka,mikakati dhaifu ya kutekeleza sheria za rushwa ya ngono na uelewa hafifu.

Hii inasababisha waathiriwa wa rushwa ya ngono kuendelea kuumia kimya kimyaa ambapo  wakosaji kuendelea na vitendo hivi bila kuchukuliwa hatua stahiki za sheria.

John Jiwenary.


Amesema ni Tafiti zinabaini kwamba tatizo la rushwa ya ngono kwenye vyuo vya elimu ya juu na vilivyoshiriki lipo na tatizo hili ni kubwa na si lakupuuza kwani Shuhuda za waathirika zimetambuliwa.

Aidha amesema rushwa ya ngono hugeuza haki ya muombwaji kuwa upendeleo na sio stahiki kwani inahusu kumpokonya mtu haki yake,kusababisha madhara kwenye nyanja mbalimbali kama vile kupata jelaha lisilo tibika kwenye maisha yake hata pahala pengine.

Muhanga anaweza kugeuzwa mtumwa wa ngono,hivyo kushindwa kukuza vipaji vyake vya uhalisia ni ukweli usiopingika  hali hii huathiri uchumi wa taifa.

John Jiwenary.

Kwa Upande wake Mwakilishi wa makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma UDOM Dkt Omben Msuya amesema hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko mengi kuhusu uwepo wa MATUKIO ya rushwa za ngono kwenye Taasisi za elimu ya juu ila katika Chuo cha UDOM tumeweka mifumo kwaajili ya kuzuia wanajamii wa Chuo cha Dodoma kujihusisha na rushwa au unyanyasaji wa Aina yoyote.

Chuo kimeimarisha kamati ya maadili iliyokuwepo tangia mwa 2009 na kamati hiyo iko wazi endapo mwanafunzi au mfanyakazi amefanyiwa vibaya kunasehemu ya kupelekea  malalamika bila kusahau masanduku ya maoni.

Dkt Msuya.


Na kuongeza kusema" lengo ya Masanduku ya maoni ni kuwapa nafasi wanafaunzi kutoa taarifa pale tu wanapokutana na vitendo hivi kwa wahadhiri wao," amesema.

Naye Mkurugenzi wa Tasisi ya huduma za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es salaam UDSM Lulu Muhai amesema wamefungua ukusanjaji wa taarifa kwa kuwa na namba ya simu kwa wanafunzi kupiga simu pindi wanapokutana na changamoto ya rushwa ya ngono kwa wahadhiri wao.



Pia amesema wameaajiri wafanyakazi 36 wa jinsia zote wakike na wanaume ambao kazi yao kubwa ni kupokea malalamiko kwa wanafunzi na baadhi ya wafanyakazi,na pia tumeandaa vipeperushi vinavyoelezea  uadilifu.


Baadhi ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina ya mkutano ulioitishwa na TAKUKURU kwa waandishi hao uliofanyika leo   jijini Dodoma.



 

Post a Comment

0 Comments