BALOZI MULAMULA ASEMA MISINGI YA SERA YA MAMBO YA NJE HAIJABADILIKA

 


📌MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amesema kuwa Misingi ya Sera ya Mambo ya Nje haijabadilika na iko imara, kusisitiza umoja na kutoshabiana kisiasa na upande wowote pamoja na kuwaunga mkono wale wote wanaokandamizwa.

Balozi Mulamula ameyasema hayo wakati alipokutana katika kikao kazi na watumishi wa Wizara ya leo Jijini Dodoma na kuwasihi watumishi kujenga mahusiano na kutekeleza kwa ufanisi Diplomasia ya Uchumi.

“Uchumi wa Tanzania unakuwa kutokana na juhudi zetu, na mtakumbuka kuwa Wizara ya Mambo ya Nje majukumu yake ni mtambuka kwani yanagusa kila sekta, na lengo la kikao hiki ilikuwa kukumbushana maagizo ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,”

“Nashukuru sana katika kukutana kwenye kikao na wafanyakazi binafsi nimehamasika na kuwa na ari mpya ya kuchapa kazi, na pia wafanyakazi wamehamasika mara baada ya kikao cha leo,” 

Katika awamu ya Sita, Serikali imefungua balozi mbili mpya na Konseli mbili na naamini kutokana na msisitizo wa Mhe. Rais Samia wa kutekeleza Diplomasia ya uchumi kwa vitendo tutaendelea kufungua balozi nyingine zaidi kadri tutakapokuwa tunapata uwezo…….kile tulichonacho tukitumie vizuri kwani milango imefunguka.

Mazingira ni mazuri na ndiyo maana tunaendelea kuhamasisha wawekezaji na wafanyabiashara kuja kuwekeza Tanzania.

Mwana Diplomasia namba moja Mhe. Rais Samia amekuwa mstari wa mbele kutusaidia katika hili na hata juzi alipokutana na mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa aliweza kuwaeleza kuwa Tanzania ipo pamoja na kwamba tunaenda wote katika  kufanikisha malengo ya watanzania yaweze kuboreka zaidi.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Nassor Mbarouk (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine pamoja na Naibu katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Fatma Rajab.


 

 

Post a Comment

0 Comments