KWA mara ya Kwanza barani Afrika, Benki ya NMB imeleta mapinduzi makubwa ya huduma ya malipo ya kidigitali kwa kutumia mfumo wa QR Code (Quick Response).
Akizungumza wakati wa Kutambulisha huduma hiyo mpya nchini kwa wafanyabiashara wa sekta ya Utalii kanda ya kaskazini, Meneja wa Mastercard Mosses Alfonce amesema kuwa huduma hiyo ni mapinduzi makubwa ya matumizi ya fedha kidigitali.
NMB na Mastercard wamekuja na huduma hii ya ‘QR pay by link’ kuhakikisha kila mfanyabishara mkubwa na mdogo ana uwezo wa kupokea malipo kutoka kwa wageni hawa bila usumbufu wala mkwamo
Alfonce.
Anachotakiwa mfanyabiashara kuwa nacho ni QR code ya malipo pekee ambayo imeunganishwa na Akaunti yake ya NMB kwa hiyo anaweza kulipwa kwa benki yoyote aliyonayo mteja duniani kwa njia rahisi, salama na haraka tena bila gharama yoyote kwa mpokeaji
Nae Mkuu wa idara ya biashara za Kadi kutoka Benki ya NMB, Philbert Casmir amesema kuwa mfumo huo unafanya kazi kwa kujaza taarifa za kadi kwa mara moja tu na kukuwezesha kutumia huduma kulipa mara nyingi atakavyo mteja.
Kikubwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo, waje NMB kuchukua hizo QR Code ya malipo kuwasaidia wateja wao wa kitaifa na kimataifa kulipa kiasi chochote cha fedha kutoka benki yoyote duniani na kuingia kwenye akaunti zao za benki ya NMB
Tumekuja kufanya ubunifu huu kwenye simu zetu wenyewe kwani imekuwa kifaa muhimu kwa maisha ya mwanadamu lakini pia imetokana na maoni ya wateja wake katika kuleta suluhu ya matatizo ya kifedha wanayokumbana nazo
Philbert.
Ameongeza kwakusema kuwa faida ya kuwa na mfumo huu wa QR Code ya malipo kupitia NMB itamsaidia mfanyabiashara kulipwa na mteja fedha kwa wakati bila usumbufu tena kutoka benki yoyote duniani tofauti na zingine ambazo zinalipa kwa benki za ndani pekee, lakini pia haina makato kwa mlipwaji bali mlipaji anakatwa asilimia tatu pekee.
Faida nyingine za malipo haya ni kujiwekea sifa ya kupata mkopo wa benki kwa urahisi kulingana na taarifa za mtitiriko wako wa mzunguko wa fedha hivyo nitoe wito kwa wafanyabiashara katika mnyororo mzima wa utalii kuhakikisha wanatumia suluhisho hili lenye manufaa makubwa
Mkurugenzi wa Chama cha waongoza Watalii Tanzania (Tato), Elirehema Maturo amesema kuwa mfumo huo utasaidia kuondoa usumbufu kwa wateja wao ambao wamekuwa wakisumbuka kuchenchi hela kwa ajili ya matumizi.
Sekta ya utalii imekuwa ikikumbwa na changamoto mbalimbali za kifedha hasa mfumo wa malipo kwa wateja wao kitendo kinachokwanza baadhi ya watalii, hivyo mfumo huo utasadia kupunguza usumbufu
Amesema kuwa sekta ya utalii bado inahitaji bunifu zaidi katika huduma za usafiri, malazi na mawasiliano na malipo, lakini pia katika ya mazao ya utalii
Ubunifu wa mara kwa mara unasaidia kukuza utalii wetu katika viwango vigine hivyo niipongeze benki ya NMB kwa kuleta mapinduzi haya ya kidigitali ambayo imekuwa na usumbufu mkubwa, amesema Maturo.
0 Comments