WANAHABARI DODOMA WAZINDUA BLOGU YAO

Rais wa Umoja wa Vilabu Nchini.Deogratius Nsokolo (Kulia) na Mwenyekiti wa CPC Mussa Yusuph (Kushoto) wakionesha leseni ya usajili ya Huduma za Maudhui ya Mtandao kutoka TCRA.

📌NA BEN BAGO

Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Dodoma (Central Press Club) kimezindua blogu yake ili kutanua wigo kwa Watanzania kupata habari za uhakika kutoka jijini humo.

Akizungumza baada ya Uzunduzi huo Rais wa Umoja wa Vilabu vya Habari Tanzania(UTPC) Deogratius Nsokolo amesema blogu hiyo ni hatua muhimu katika ukuaji wa tasnia ya habari jijini Dodoma.
Nsokolo ambaye yupo jijini hapa katika ziara ya siku moja ya kikazi kukutana na kamati tendaji ya CPC pamoja na baadhi ya wanachama amesema uwepo wa blogu hii utawawezesha waandishi kuwa na jukwaa la uhakika la kuchapisha habari zao.

“Kuna muda tunaandika habari zetu lakini zinakosa nafasi huko kwingine,hivyo blogu hii itakuwa mkombozi kwa waandishi.” Amesema Nsokolo.
Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo akisisitiza jambo kwa baadhi ya Wanachama wa CPC.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa CPC,Mussa Yusuph amesema uwepo wa blogu hiyo ni jukwaa la wanahabari kutimiza majukumu yao ipaswavyo kwa kuhakikisha taarifa muhimu zinawafikia wananchi, lakini pia kuibua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ili ziweze kutatuliwa na mamlaka husika
Usajili wa blogu hii umekamilika ikiwa ni jitihada za UTPC kusaidia vilabu vya habari nchini kuwa na blog ili kurahisisha upatikanaji wa habari kwa wananchi katika katika zama hizi za kidigitali ambako kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Watanzania zaidi ya milioni 2 wanatumia mitandao kupata habari.

Pia katika hatua nyingine Nsokolo amezindua zoezi la ugawaji wa vifaa vya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa corona kwa kuwakabidhi vifaa baadhi ya wanachama wa CPC.
Vifaa hivyo ambavyo pia vimetolewa na UTPC kwenda kwa Wanachama ili viwasaidie kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.

Mwanachama wa CPC Saida Issa akipokea vifaa vya kujikinga na Corona kutoka kwa Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo.Katikati ni Mwenyekiti wa CPC Mussa Yusuph.


Mwanachama wa CPC Daniel Mkate akipokea vifaa vya kujikinga na Corona kutoka kwa Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo.Katikati ni Mwenyekiti wa CPC Mussa Yusuph.Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo akiwa katika picha ya pamoja na Kamati Tendaji na baadhi ya Wanachama wa CPC baada ya kikao.

Post a Comment

0 Comments