📌AMISA
AMIRI & WILSON JOHN.
WATANZANIA
wametakiwa kubadilisha mtazamo hasi kuhusu watu wanaojishughulisha na shughuli
za uokotaji wa chupa za plastiki na kuchukulia shughuli hiyo kama fursa ya
kujipatia kipato cha kuendesha maisha na kukuza uchumi.
Kauli
hiyo imetolewa Jijini Dodoma na Mnunuzi wa chupa za plastiki Bi. Khadija Zuber
wakati akizungumza na CPC Blog ambapo amesema watu wengi wamekuwa na mitazamo
tofauti tofauti kuhusu biashara ya chupa za plastiki wengi wakiwachukulia kama
wahuni au vibaka
Amesema jamii inatakiwa kuwa na mwamko juu ya
biashara ya chupa za plastiki kwani ni ajira isiyokuwa na mtaji na ni rahisi
kujipatia kipato.
Mimi ni mfanyabiashara ambaye najihusisha na biashara ya chupa za plastiki katika mtaa huu wa Majengo ambapo tunanunua chupa hizi na kuzipeleka kiwandani kwa ajili ya uchakataji na zikishachakatwa tunapata bidhaa mbalimbali kama majagi, nguo za tetroni, na bidhaa nyingine nyingi
Niiombe jamii na serikali kwa ujumla kwani tumekuwa tukihangaika kupata eneo la kudumu ili kuendesha biashara hizi, na jamii iamke sasa kwani biashara hii inasaidia hata majumbani kutunza mazingira kwani inasaidia kuweka mazingira safi na salama
Khadija
Kwa upande wake muokota machupa James Andrew
amesema amekuwa akipambana na changamoto nyingi katika uokotaji wake ikiwemo
kudharauliwa, kutukanwa na jua kali wakati wa kuzunguka mitaani pia amesema
changamoto nyingine ni bei kuwa ndogo ya ununuzi ambapo kilo moja ya chupa ni
sh.mia mbili (200) hivyo haikidhi
mahitaji
Tunaomba serikali na wanunuzi kuthamini kazi yetu, waone ni jinsi gani tunakumbana na changamoto katika kutafuta chupa ambapo serikali ikithamini na kuona mchango wa hii kazi katika usafi wa mazingira
Marighafi hii inasaidia kupata bidhaa kadha wa kadha hivyo tunaomba jamii kwa ujumla watambue umuhimu wetu na mchango wetu katika upatikanaji wa hizi bidhaa kama vyombo vya plastiki, chupa za maji na nguo
Andrew
0 Comments