ASASI ZA ZA KIRAIA ZAHASWA KUTOJIHUSISHA NA SIASA





📌NA HAMIDA RAMADHANI


WITO umetolewa kwa Watetezi wa Haki za Binadamu kutojihusisha na shughuli za kisiasa ili kuondoa dhana ya kutambulika kama wanasiasa.

Hayo yameelezwa leo na Mratibu wa Mtandao wa Wawatezi wa Haki za Binadamu Tanzania  Onesmo Olengurumwa wakati akizungumzwa na waandishi wa habari katika kikao kilichokua kinaeleza hali ya utetezi wa haki za binadamu kanda ya kati.

Olengurumwa amesema watetezi wa haki za binadamu kujihusisha na siasa ni kutengeneza mkanganyiko kwa wananchi wenye itikadi tofauti  ndani ya vyama vyao.

Ili kuondoa mkanganyiko baina ya watetezi wa haki za binadamu na serikali hakuna haja ya kuweka vitu viwili kwa wakati mmoja kama ni mtetezi wa haki za binadamu baki kuwa mtetetzi na kama ni mwana siasa baki kuwa mwana siasa
Olengurumwa.

Kwa upande wake Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Dodoma William Mtwazi amesema kuwa kwasasa tupo kwenye kipindi cha uchaguzi hivyo kila mmoja lazima ahakikishe anazingatia misingi sheria na kanuni za uchaguzi zilizowekwa ili kulinda haki zetu.

Hata hivyo ziara ya mratibu huyo Taifa,ametembelea mashirika na wanachama wa mtandao kanda ya kati na ilianza Julai 16 hadi 20 katika Mikoa  ya Kanda ya kati ilijumuisha Singida Morogoro na Dodoma .

Post a Comment

0 Comments