BRAZIL YAFIKISHA VIFO ZAIDI YA 70,000 KUTOKANA NA VIRUSI VYA CORONA

Brazil imefikisha vifo 70,000 kutokana na virusi vya corona jana Ijumaa, wizara ya afya imesema, licha ya kuwa idadi ya vifo kwa siku inaonekana kuimarika.

Wizara imesema kumekuwa na maambukizi mapya kwa watu 45,000 na vifo1,200 katika masaa 24 yaliyopita, na kufikisha idadi jumla ya kesi milioni 1.8 pamoja na vifo 70,400.

Brazil nchi yenye wakaazi milioni 212, ni ya pili kuathirika vibaya na janga la maambukizi ya virusi vya corona duniani baada ya Marekani.

Idadi ya watu waliofariki imeongezeka mara dufu katika siku 35 zilizopita ambapo majimbo ya Sao Paulo na Rio de Janeiro yameathirika zaidi, yote kwa pamoja yakiripoti vifo 17,400 na 11,200.

DW SWAHILI,

Post a Comment

0 Comments