BREAKING NEWS: JPM RASMI KUKEPEPERUSHA BENDERA YA CCM UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2020

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa unaoendelea jijini Dodoma wamempitisha kwa kishindo kupitia kura za ndiyo Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kwa awamu ya pili kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu 2020.

Wajumbe wote 1,822 walioshiriki mkutano huo jijini Dodoma leo Julai 11, 2020 wamempigia Dkt. Magufuli kura za ndiyo ikiwa ni ushindi wa asilimia 100.

Hivyo,kwa mara nyingine Dkt.Magufuli ataingia ulingoni kupambana na Wanachama wa watakaochaguliwa na Vyama vingine vya Upinzani kusaka ridhaa ya Watanzania kuwaongoza katika nafasi ya Urais.

Post a Comment

0 Comments