📌HAMIDA
RAMADHANI
VIONGOZI
mbalimbali na makundi maalumu Mkoani Dodoma wamekutana na kuazimia kwa kauli
moja kuwa chachu katika kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuwapeleka wajawazito Kliniki.
Makundi hayo
yaliyojumuisha waelimishaji kutoka sekta ya Afya,wajasiriamali wadogo
wadogo,viongozi wadini na waganga wa tiba mbadala wamekutana kwa lengo la
kuhamasisha jamii kuwapeleka wajawazito na watoto wachanga Kliniki ili
kupunguza vifo vifo vinavyoweza kuepukika
John Yuda ni
mwezeshaji na Mratibu wa mpango wa Taifa wa huduma za Afya mashuleni amesema
Kutokana na kuibuka kwa mlipuko wa virusi vya Corona umeleta athari nyingi
kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya afya ambapo imepelekea wamama wajawazito
kutohudhuria Kliniki
Kwa upande
wake Mratibu wa huduma za mama na mtoto Mkoa wa Dodoma Nice Mosha amesema
kutokana na virusi vya Corona watu walikuwa wakiogopana huku wengine kutoona
umuhimu wa kwenda Kliniki ambapo kumekuwepo na athari za kiafya kwa mama na
Mtoto kutokana na kutokufata huduma za afya
Nao baadhi ya
washiriki akiwemo kiongozi wa Kanisa la Rehoboth Mchungaji Edward Mbwambo na
Rahel Moleli ambaye ni Muhudumu wa afya ngazi ya Jamii wao wameahidi kwenda
kutekeleza maadhimio walioadhimia kikamilifu
0 Comments