DODOMA MAMBO NI MOTO! FOUNTAIN GATE FC YATINGA LIGI DARAJA LA KWANZA



📌NA BEN BAGO

TIMU ya soka ya Fountain Gate FC ya jijini Dodoma iliyokuwa inashiriki ligi Daraja la Pili (SDL) imefanikiwa kupanda daraja na sasa ni rasmi msimu ujao inakwenda Ligi Daraja la Kwanza kuwania kupanda ligi kuu ya Tanzania Bara.

 Timu hiyo inayomilikiwa na shule za Fountain Gate Academy imefika hatua hiyo baada ya kuifunga African Sports kwa penati 3-1 kwenye mchezo wa nusu fainali uliyofanyika leo katika uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.Timu hizo zilimaliza dakika 90 za mchezo wa Nusu Fainali zikitoka sare ya bila kufungana.

Akizungumza na kipindi cha michezo cha E-Sports cha E-FM Meneja wa timu hiyo Wendo Makau amesema siri ya mafanikio hayo ni nidhamu,mazoezi na mipango iliyowekwa na uongozi wa timu hiyo.

Wendo amesema hawatoivunja timu hiyo japo kuna mipango kidogo ya kuziba mapungufu yaliyopo ili kwenda kupambana ikiwa lengo ni kucheza ligi kuu.
Meneja huyo amewashukuru wakazi wa Dodoma kwa ushirikiano walioutoa tangu kuanzishwa kwa kituo hicho cha soka.

Tangu tuanzishe timu hii wana Dodoma wametuunga mkono,tunawashukuru sana lakini kazi haijaisha bado tunahitaji ushirikiano wao ili tuendelee na mapambano.
Wendo Makau,Meneja Fountain Gate FC

Post a Comment

0 Comments