NA RAMADHAN HASSAN
MAMLAKA ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)
imejipanga kuhakikisha kwamba mafuta yanapatikana kwa wingi wakati wa kipindi
cha uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu
ambapo meli mbili zinatarajia kuingiza
mafuta mwezi ujao.
Pia,imesema kwamba sababu ya kuadimika kwa mafuta ni
kutokana na janga la ugonjwa wa Corona ambapo kwa sasa mambo yamekaa vizuri na
mafuta yatapatikana kwa wingi.
Hayo yamelezwa Jijini hapa na Meneja Mawasiliano na Uhusiano
wa Mamlaka hiyo,Titus Kaguo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini
hapa.
Kaguo amesema Ewura
imejipanga kuhakikisha kwamba mafuta yanapatikana katika kipindi cha uchaguzi
wa Oktoba mwaka huu.
Meneja huyo amesema Juni mwaka huu matumizi ya mafuta yalipanda kwa
asilimia 7% na Julai yakapanda kwa
asilimia 12 kutokana na ugonjwa wa Corona.
“Moja ya kazi ya Ewura ni kuhakikisha wakati wa kampeni
mafuta yanapatikana kwahiyo mtu yoyote ambaye ataingia hapa katikati na
kuingilia biashara ya mafuta huyo ana malengo ya kuvuruga uchaguzi na sisi
hatutakubali.Na adhabu kubwa ni kukufuta leseni”
Kama kuna mfanyabishara anafanya visivyo tutamchukulia hatua kali,lakini meli ya dharua iliingia tarehe 13 mwezi wa saba ilikuwa na lita milioni 28 lakini pia kati ya 27 mwezi huu na tarehe 3 mwezi wa nane itaingia meli yenye mafuta ya lita milioni 89 ambazo hizo kwa mahitaji ya kawaida yanaweza kwenda kwa siku 20.
Amesema pia tarehe 10 mwezi wa nane itaingia meli yenye
ujazo wa mafuta lita milioni 67 kuziba
pengo ambalo limeonekana.
“Pia Mamlaka inayoingiza mafuta nchini tumeiagiza mwezi wa
nane iingize meli mbili za mafuta na hii
tunafanya kwa kuwa tunaenda katika mchakato wa kampeni na uchaguzi ili
wakati huo kuwe kuna mafuta.
Amesema Ewura
imechunguza na kugundua kwamba kuna baadhi ya wafanyabiashara ambao sio
waaminifu wanaficha mafuta ili waweze kupata faida.
Sasa hili tumeishaling’amua kuna eneo watu wanapiga kelele kwamba mafuta hakuna, wiki mbili kuna mtu alinipigia simu kutoka Ifakara alisema alinunua lita moja kwa shilingi 7000 nawaambia tutawakamata mmoja baada ya mwingine na adhabu yake atakayochukuliwa atajuta maishani
0 Comments