HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA(BMH) KUWA KITOVU CHA UPANDIKIZAJI WA FIGO AFRIKA




📌NA HAPPINESS MTWEVE

HOSPITALI ya Benjamini Mkapa(BMH) inatarajia kuwa kitovu ch upandikizaji wa figo Afrika Mashariki kwa kutumia wataalam wa ndani.

Akitangaza mafanikio hayo yanayoendelea kupatikana katika serikali ya Awamu ya Tano chini, ya rais, Dk.John Magufuli, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Alphonce Chandika, alisema wamepiga hatua kubwa katika eneo hilo.

Dk.Chandika alisema, wamefanikiwa kupandikiza figo kwa mgonjwa mwingine tangu walipofanikiwa kufanya hivyo kwa mgonjwa wa kwanza 2018 na kufanya mgonjwa huyo kuwa wa pili kwa kutumia wataalam wa kitanzania.

"Sisi watumishi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, wanaunga mkono juhudi za rais, DK.Magufuli kwa vitendo, wanataka kuhakikisha wanakuwa kitovu kwa Nchi za Afrika,"alisema.

Alisema, mafanikio hayo yamewezesha kuokoa kiasi kikubwa Cha fedha kilichokuwa kikitumiwa na watanzania waliokuwa walienda kupandikizwa figo nje ya nchi na hivyo kusaidia ukuaji wa uchumi.

Mkurugenzi huyo alieleza kuwa jumla ya wagonjwa 75 wanaendelea kupatiwa huduma ya matibabu ikiwemo usafishwaji wa figo.

Dk.chandika aliwaasa watanzania kuwa na tabia ya kupima afya zao badala ya kusubiri kuwa na Hali mbaya ndipo wafike hospitali kupatiwa huduma.

"Sababu ya kufikia hatua ya kupandikizwa figo na kusafishwa zinafahamika ambapo moja wapo ni mawe kwenye figo na kwenye mirija ya kibofu cha mikojo, ambapo hapa hospitali tuna mashine ya kuyeyusha mawe hayo hivyo ukiwahi mapema na kupatiwa huduma si rahisi kufikia hatua ya kusafishwa ama kupandikizwa figo,"alisema.

Kwa upande wake, mganga mbobezi wa magonjwa ya Figo, katika hospitali hiyo, Keissy Shija, alisema, huduma hizo za upandikizaji na usafishaji wa figo zitakuwa endelevu na zitakuwa huduma za kawaida za kila siku kama nyingine.

Shija alisema, mpaka sasa wamepandikiza Figo watanzania 11 kwa ushirikiano na wawili kwa kutumia wataalam wa ndani hivyo kuwa na idadi ya watanzania 13 waliopandikuzwa figo ambao wote kwa asilimia kubwa afya zao zinaendelea vizuri.

Profesa. Ipyana Mwampagatwa, Akizungumza kwa niaba ya Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dodoma(UDOM), alisema, waliweka malengo ya miaka mitano kuanza kutoa huduma hiyo kwa kutumia wataalam wandani lakini ndani ya miaka miwili wameweza kukufanikisha hilo, ni hatua kubwa sana ambalo lilihitaji udhubutu.

Mwampagatwa, alitoa wito kwa BMH, kuongeza juhudi katika eneo hilo ili waweze kusaidia kusambaza ujuzi katika hospitali nyingine ndani ya Tanzania na afrika Mashariki kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments