KIFO CHA JOB LUSINDE: FAMILIA YATOA NENO,HISTORIA YAKE KWA UFUPI


📌DOTTO KWILASA

ALIYEKUWA mwanasiasa mkongwe ambaye pia alikuwa Waziri katika baraza la kwanza la  Mawaziri baada ya Uhuru,Mzee Job Malecela Lusinde, ambaye ni ndugu wa Mh. John Samwel Malecela,amefariki dunia .

Mzee Lusinde ni waziri pekee aliyebaki katika Baraza la Mawaziri la kwanza baada ya nchi kupata Uhuru.

Aidha kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wanafamilia ya marehemu,mwili wa  balozi mstaafu Lusinde unatarajiwa kuwasili kesho mkoani hapa kwa ajili taratibu za maziko.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Jijini hapa,msemaji wa familia mbaye ni Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Malechela ambaye pia ni kaka wa Marehemu amesema taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwake Jijini Dodoma.

Marehemu mdogo wangu  Mzee LUSINDE amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo Jijini Dar es Salaam alipokuwa anapatiwa matibabu,ni pigo kwa familia.

John Samuel Malecela.

Akimzungumzia marehemu enzi za uhai wake mzee Malechela amesema, Mzee Lusinde atakumbukwa kwa utendaji kazi uliotukuka,uzalendo kwa nchi yake kupitia nafasi mbalimbali alizozitumikia.

Enzi za uhai wake marehemu Mzee Lusinde pia amewahi kuwa mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Dodoma

Naye mjumbe wa baraza la wazee wa CCM Mkoa wa Dodoma  Mzee Peter Mavunde amemuelezea Mzee Lusinde kuwa ni mtu aliyekuwa mwaminifu kwa chama na serikali yake.

Kwa upande wake Mbunge wa Dodoma Mjini Anthoni Mavunde ambaye ni Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Vijana amemuelezea Mzee Lusinde kama mtu aliyechangia yeye kuwa Mbunge kutokana na ushauri wake alioutoa kwake.


HISTORIA YAKE KWA UFUPI:


Mzee Lusinde  alizaliwa  Kikuyu, Dodoma tarehe 10/9/1930

Marehemu Lusinde alisoma shule ya msingi ya misheni, baada ya kufaulu vizuri, alichaguliwa kujinga na shule ya sekondari ya Alliance Sec. School. Shule hiyo ilikuja kubadilishwa jina na kuitwa Mazengo Sec. School"(jina la Chifu maarufu wa Kigogo).

Hata hivyo baadae miaka ya mwisho ya 1940s, alifaulu mtihani wake na hivyo akaendelea na masomo 'Tabora Boys Sec. School', shule ambayo wamesoma idadi kubwa ya viongozi wa mwanzo wa Tanzania.

Post a Comment

0 Comments