KIMEELEWEKA! DODOMA JIJI FC YAPANDA LIGI KUU,WAZIRI MKUU ASHUHUDIA IRINGA UNITED 'WAKIPOKEA KICHAPO'



📌NA BEN BAGO

TIMU ya Dodoma Jiji FC (DJFC) imefanikiwa kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga timu ya Iringa United mabao 2:0 katika uwanja wa Jamhuri,mchezo ambao umeshuhudiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Dodoma Jiji ilihitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kwanza katika kundi B ambalo lilikuwa na upinzani mkali kati ya DJFC na timu ya Ihefu FC ya Mbarali Mbeya.



DJFC na Ihefu zote zimemaliza ligi zikiwa na alama 51 baada ya michezo 22 lakini DJFC wameongoza kundi hilo kwa utofauti wa magoli 4 baada ya michezo ya leo ambako Ihefu wameifunga Cosmopolitan ya magoli 3:0.

Baaada ya ushindi huo Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ambao ndio wanamiliki timu ya DJFC amesema licha ya wao (Jiji) kuwekeza kwenye timu hiyo lakini DJFC ni ya wana Dodoma wote hivyo lazima wajivunie mafanikio ya timu hiyo.

Kunambi amesema uwekezaji walioufanya msimu huu kwenye timu hiyo ni mwanzo tu wa mipango ya jiji la Dodoma kuendeleza michezo.

Soka ni uwekezaji,huu ni mwanzo tutawekeza zaidi kuhakikisha tunakuwa na timu imara ya kupambana kwenye ligi kuu msimu ujao.
Godwin Kunambi,Mkurugenzi Dodoma Jiji











Post a Comment

0 Comments