📌NA MWANDISHI WETU
Baadhi ya Wagombea wa nafasi udiwani viti maluum kupitia Jumuiya
ya Wanawake wa Chama cha Maapinduzi (UWT) wilaya ya Mpwapwa wamelalamikia
vitendo vya Rushwa kutawala katika uchaguzi hizo.
Mmoja wa Watia Nia katika nafasi ya Udiwani viti maluum ambae hakutaka jina lake
kufahamike amesema baadhi ya wagombea
wametumia fedha kuwanunulia chakula na vinywaji
Wajumbe ili waweze kuchaguliwa.
Kufuatia kura hizo za maoni zilizofanyika katika viwanja vya
CCM wilaya hapa,Chama Cha Mapinduzi kimepata wagombea wanaotarajiwa kupambana
na vyama vingine vya siasa katika uchaguzi Mkuu mwishoni mwa mwezi Oktoba ili
kupanda masiwani watakao unda baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya
Mpwapwa.
Baraza hilo litakuwa
na Madiwani 46 wakiwamo 33 Madiwani wa
Kata na Madiwani 13 viti maluum kutoka katika Tarafa zote za Wilaya ya Mpwapwa.
Mmoja wa wagombea Grolia Manyemba Tarafa ya Kibakwe akionyesha namba yake ya kura kwa Wajumbe hawapo pichani. |
Waliongoza kura za maoni ni Nelly Kaguri,(429) Shani Bilali (306)Rehema Vahaye (300) na Mariam Makasi (263)
Wakati majina mengine ni Juliana Ninde (296)Nowadia Lumambo
(372) na Dorisia Fweda (200) Sophia Chidalamai (371) na
Maria Kigosi kura 391.
Wengine ni Grolia Manyemba 290,Zelly Ngowo 232,Frida Nyoka
na Rehema Mtinangi 248.
Aidha Madiwani 3
wameshidwa wakitete nafasi zao na kujikuta Wajumbe wakiwatoa nje ya mfumo
ambao ni Devota Samweli, Pamela Mnemele, na Teresia Wolle.
Wakati Madiwani wa 7 waliweza kutetea nafasi zao na kurudi
tena kwenye kinyang'anyiro. Msimanizi wa uchaguzi huo bwana Henry Mwenge Katibu
Mwenezi mkoa wa Dodoma amesema huo ni mchakato wa awali na kuwataka wagombea
kuwa watulivu wakisubiri maamuzi ya vikao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uchaguzi wa wilaya ya Mpwapw Jackson
Shiluh amesema kuhusu vitendo vya Rushwa kama kuna mgombea ana ushahidi wa tuhuma
wanazo zitoa,wapeleke ofisini na yatasikilizwa na kufanyiwa kazi malalamiko
hayo.
Naye mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri
amewataka wagombea udiwani wazalendo katika kutetea maslahi mapana ya Kata zao
wilaya na Taifa kwa ujumla.
0 Comments