KURA ZA MAONI DODOMA: DIWANI KILIMANI APETA,AKUSANYA ZAIDI YA NUSU YA KURA ZOTE




📌NA BARNABAS KISENGI

Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kilimani jijini Dodoma,Neema Mwaluko  ameongoza katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata hiyo.

Katika zoezi hilo la kura za maoni lililofanyika leo tarehe 25 Julai 2020,Neema Mwaluko amepata kura 35, na  mpinzani wake Steven Mwanga amepata kura 7.

Wagombea wengine waliojitokeza kutia ni ya kuwaikilisha CCM katika Uchaguzi utakaofanyika baadaye mwezi Oktoba ni  Janeth Chicago aliyepata kura 4, Fatima Mbwana Kura 4, Yusufu Mikono kura 0, Charles Bupilipili(0), Maximilian Rutebeka kura 0.


Katika zoezi hilo ndani ya kata ya Kilimani Wajumbe waliopiga kura ni 53,ambapo Neema Mwaluko ametia nia kutetea kiti chake.

Post a Comment

0 Comments