MAAGIZO YA JPM TAKUKURU: TISA WASIMAMISHWA KUPISHA UCHUNGUZI


📌NA DOTTO KWILASA

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) imeunda Tume huru toka nje ya taasisi hiyo itakayochunguza matumizi ya pesa yaliyotumika katika Majengo Saba Pamoja na kuchunguza iwapo kuna ubadhirifu ,wizi au rushwa zilizotumika katika ujenzi huo.

Majengo hayo ya TAKUKURU yapo katika wilaya za Chamwino na Mpwapwa Mkoani Dodoma,Ngorongoro Mkoani Arusha,Manyoni Mkoani Singida,Masasi Mkoani Mtwara,Namtumbo Mkoani Ruvuma pamoja na Ruangwa Mkoani Lindi.

Hatua hii imekuja kufuatia hoja za mapendekezo zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli dhidi ya taasisi hiyo yaliyolenga kuondoa madoa ya uwepo wa viashiria vya rushwa.

Hivi karibuni Rais Magufuli wakati wakati akizindua jengo la TAKUKURU ngazi ya wilaya lililopo katika wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma aliiagiza taasisi hiyo kuona haja ya kujitathimini kwa dhidi ya tuhuma za  viashiria vya rushwa kwa baadhi ya watumishi wake .



Akiongea na vyombo vya habari Jijini hapa,Mkurugenzi Mtendaji wa TAKUKURU Brigedia Jenerali  John Mbung'o amesema taasisi hiyo imeunda timu itakayotokana  na wajumbe wanne kutoka taasisi ya Contractors Registration Board,Suma Construction Company Limited na Tanzania Building Agency.

Uchunguzi huu utafanyika kwa siku kumi na nne kuanzia Sasa na tuhuma zozote zitakazothibitika zitachukuliwa hatua Kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.
Brigedia Jenerali  John Mbung'o

Mkurugenzi huyo wa TAKUKURU amesema ili kufanya uchunguzi uwe wa haki, amechukua uamuzi wa kuwasimamisha kazi watumishi wote wa kitengo Cha usimamizi wa miliki ambao walihusika Katika ujenzi na usimamizi wa Majengo hayo.

Amewataj watumishi hao waliosimamishwa kupisha uchunguzi kuwa wapo tisa ambao  ni January Nyakongeza,Adam Mandia, Fortunatus Ngailo,Mohamed Kichewele,Nathaniel Otieno,Wilhelm Chuwa ,Hamis Masoud ,Mbwana Malumbo na Benedict Mabula.


Nimekivunja kitengo cha usimamizi wa miliki (Estate Management Unit) TAKUKURU ili kiweze kisukwa upya na kuwa na ufanisi zaidi.
Brigedia Jenerali  John Mbung'o

Post a Comment

0 Comments