NA HAMIDA RAMADHANI
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt.Rehema Nchimbi amesema, wanatarajia kumpa tuzo Rais Dk,John Magufuli kwa kuinua zao la Mkonge hapa nchini kabla ya kumaliza kipindi chake cha pili cha uongozi.
Dkt.Nchimbi
ameongea hayo leo katika kikao cha wadau wa zao la Mkonge kilichofanyika Jijini
hapa, ambapo kwa kauli moja walikubaliana kuweka mikakati wezeshi kwa kwa ajili
ya kuinua zao hilo kurudi kama zamani.
Nasema hivi sisi tutampa tuzo ya kuinua zao la mkonge hapa nchini Rais Dk,John Magufuli kabla muda wake wa uongozi kumalizika, kwani tuna kila sababu ya kufanya hivyo
Dkt.Nchimbi.
Aidha Dkt.Nchimbi amesema kuwa kama mambo makubwa
ambayo hayakuwezekana kufanyika katika kipindi kifupi cha utawala wake Rais
Magufuli yamefanyika kwanini zao la Mkonge ishindikane wakati kuna kila kitu
kinachohitaji kukuza zao hilo.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa, zao la
Mkonge miaka ya nyuma ndio lilikuwa linaongoza kwa kuliongezea Taifa mapato,
hivyo watahakikisha wanatumia mbinu zilezile kulirudisha zao hilo katika chati
hapa nchini.
‘’Kipindi cha nyuma zao la mkonge
lilikuwa linaongoza kwa kuliongezea mapato Taifa kwa asilimia 65, hivyo mkakati
uliopo sasa ni kulirudisha zao hilo na
kushika nafasi ya kwanza katika uzalishaji hapa nchini’’, amesema Mkuu huyo wa
Mkoa wa Singida.
Aidha nchimbi amesema katika utawala huu
wa Magufuli mambo ambayo yalidhaniwa hayawezekani lakini yamewezekana hivyo
Mkuu huyo amesema Mungu huyo huyo aliyemuwezesha Magufuli kuufanya Jiji la
Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi, ndiyo huyo huyo atakayesaidia kufufua zao la
Mkonge hapa nchini.
Unajua hapa Dodoma ndio madhabau ya Rais Magufuli ambaye alimuomba Mungu yakafanyika mambo makubwa katika muda mfupi, sasa na sisi tutumie madhabau hiyo hiyo kukufufua za la MkongeDkt.Nchimbi.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge
Saad Kambona amesema kuwa wameweka mkakati ya kuinua zao hilo kwa kuwashawishi
Wakulima wadogo kulima zao hilo ili uzalishaji uongezeke kwa kasi.
‘’Unajua baadhi ya watu wanafikiri
kilimo cha Mkonge kinafanywa na Wakulima wakubwa tu, siyo kweli, hata wakulima
wadogowadogo wakifanya kilimo hicho kwa wingi uzalishaji utakuwa mkubwa na
Serikali itaongeza pato la Taifa’’, amesema Kambona.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa hivi sasa
wanazalisha tani 36,000 tu, lakini
mkakati uliopo ni kuzalisha tani 120
hadi 150 kwa mwaka na inawezekana Kambona alitoa mfano wa Brazil ambayo ndiyo inaongoza kwa kilimo cha
Mkonge kwa kuzalisha tani 150 hadi 200 ambao Wakulima wadogo ndiyo wanazalisha
kwa wingi zao hilo, ikifuatiwa na Tanzania ambayobado inasuasusa.
Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa ameenda Tanga kuunda Bodi mpya ya Mkonge na kurudisha baadhi ya mali na mashamba ya
Bodi ya Mkonge zilizokuwa zimetaifishwa na baadhi ya mafisadi.
Naye Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba
amesema serikaliina mpango wa kuinua zao la mkonge hapa nchini ili kuhakiisha linafikia
malengo waliojiwekea.
Amesema haitakuwa tayari kuona waliopewa
viwanda wanaviatamia badala ya kuviendeleza ili kuwasaidia wakulima wamkonge
hapa nchini.
Serikali haitakuwa tayari kuwavumilia wenye viwanda ambavyo hawavifanyii kazi,tayari nimemuagiza Msajili Hazina aanze kuwasaka wanaoatamia viwandaMgumba.
0 Comments