Mbwa wa kuranda randa mitaani nchini Msumbiji wamekua wakifukua
makumi ya makaburi ya watoto katika maziko ya mji wa Chimoio, wakaazi
wameambia kituo cha runinga cha Miramar.
Mama mmoja amesema
siku chache zilizopita baada ya kumzika mwanawe ,alienda makaburini
kufanya usafi lakini alipofika hapo alipata mbwa tayari wamefukua na
kula maiti ya marehemu mwanawe.
Ripoti za vyombo vya habari nchi
humo zinaonesha vipande vya nguo na , mifupa na nyama ya binadamu
iliotapakaa katika eneo la makaburi ya umma.
Mwandishi wa kituo
cha runinga cha Miramar ameiambia BBC kwamba katika kipindi cha wiki
tatu makaburi 343 ya watoto yalifukuliwa na mbwa.
Wakaazi wanasema
mbwa hao wamekuwa tatizo la la kila siku na kwamba hali imekuwa mbaya
zaidi katika miezi ya hivi karibuni kwa sababu ni watu wachache
wanaoruhusiwa kufika katika maziko hayo kutokana na mlipuko wa virusi
vya corona
Janga la virusi vya corona pia limewafanya watu
kupoteza kazi na huenda hawana uwezo wa kukimu familia zao wala
kuwalisha wanyama wao.
Hatua ya makaburi ya umma kutozungushiwa au imesemekana kuchangia tatizo hilo wenyeji wanasema.
Mamlaka
ya mji wa Chimoio, ambao ni makao makuu ya mkoa wa Manica karibu na
mpaka wa Zimbabwe, haikuwepo kutoa tamko kuhusiana na hali hiyo.
BBC SWAHILI
0 Comments