RAIS DKT. MAGUFULI AENDA KUTOA POLE NYUMBANI KWA MAREHEMU BALOZI JOB LUSINDE
July 09, 2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akiandika kwenye kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha
aliyewahi kuwa Waziri katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Serikali ya
Awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere Marehemu Balozi Job
Lusinde aliyefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Msemaji wa Familia ya
Marehemu Balozi Job Lusinde, Waziri Mkuu Mstaafu John Samweli Malecela
wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa Marehemu Balozi Lusinde
Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 09 Julai 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mke wa Marehemu
Balozi Job Lusinde, Mama Sara Lusinde aliyekaa katikati mwenye kilemba
cheupe mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kutoa pole nyumbani kwa
Marehemu Balozi Lusinde Uzunguni jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Msemaji wa Familia ya
Marehemu Balozi Lusinde, Waziri Mkuu Mstaafu John Samwel Malecela mara
baada ya kutoa pole Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 09 Julai 2020.
Post a Comment
0
Comments
Hey there, We are Blossom Themes! We are trying to provide you the new way to look and use the blogger templates. Our designers are working hard and pushing the boundaries of possibilities to widen the horizon of the regular templates and provide high quality blogger templates to all hardworking bloggers!
0 Comments