Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
BENKI ya Dunia imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 50 duniani za uchumi wa kipato cha kati, ikiwa ni ya pili baada ya Kenya katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, baada ya ukuaji wa uchumi unaosukuma pato la mwananchi kukua (Per capita GNI) mwaka 2020.
BENKI ya Dunia imeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 50 duniani za uchumi wa kipato cha kati, ikiwa ni ya pili baada ya Kenya katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, baada ya ukuaji wa uchumi unaosukuma pato la mwananchi kukua (Per capita GNI) mwaka 2020.
Tanzania imeingia kwenye uchumi wa kati
miaka mitano kabla ya lengo la Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025,
jambo ambalo ni la kujivunia.
Akizungumza katika Mkutano na waandishi
wa habari leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema
kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, 2025 katika ukurasa wa pili,
kipengele 1.2
“Uchumi wa kipato cha kati umehusishwa na kuwa na nchi ambayo umaskini unapungua, uchumi imara unaojengwa na kuimarika kwa uzalishaji viwandani unaimarika na wananchi wanapata maendeleo”.
Dkt. Abbasi alisisitiza kuwa uchumi wa
kipato cha kati umegawanyika katika madaraja mawili daraja la chini
ambapo ni kuanzia dola za Kimarekani 1036 hadi 4045 na daraja la juu ni
dola 4046 hadi 12,535 na mwaka huu Tanzania imepanda daraja kuwa uchumi
wa kipato cha kati daraja la chini, pamoja na nchi za Algeria na Benin.
Aidha, Dkt. Abbasi alifafanua siri 10
zilizoisaidia Tanzania kutajwa kufikia daraja la uchumi wa kipato cha
kati na Benki ya Dunia hapo Julai 1, 2020 kuwa ni nchi yenye amani na
utulivu, na hivyo ni msingi muhimu nyuma ya mafanikio ya nchi ya
Tanzania kuingia katika uchumi wa kipato cha kati kwani bila amani
hakuna kufanyakazi, hakuna kuzalisha na hakuna kuongeza kipato. Na hivyo
viongozi, wanahabari na wananchi kwa ujumla wamesisitizwa kuwekeza
akili zao katika kuimarisha amani iliyopo na kukataa chokochoko zozote
zile zinazoweza kuharibu misingi ya maendeleo.
Siri ya pili ni mipango thabiti ya
maendeleo, ambapo Dkt. Abbasi alisema kuwa moja ya kanuni muhimu ya
kuendelea ni kuwa na mipango inayokuwekea malengo makubwa (Olympic targets).
Serikali itaendelea kuweka mipango mbalimbali ya maendeleo ya muda
mrefu na mfupi, akitolea mfano mwaka 2020 Serikali ilianza kutekeleza
Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 ambayo moja ya malengo ni kufikia
uchumi wa kati.
Kwa mujibu wa Dkt. Abbasi siri ya tatu
ni utekelezaji usioyumba, katika miaka 59 ya Uhuru na mitano ya Awamu ya
Tano Serikali imejitahidi kusimamia eneo hilo kwa kuhakikisha mipango
inayowekwa inatekelezwa kwa kina (3feet implementation).
Siri nyingine ni maamuzi magumu,
Siri nyingine ni maamuzi magumu,
“Moja ya mafanikio ya Serikali ya Tanzania kwa Awamu zote na sasa tumeimarisha katika Awamu ya Tano ni wakati fulani Serikali kufanya uamuzi mgumu ambao wakati fulani ulionekana kuwa ni ndoto lakini baadaye ukaleta mafanikio makubwa kwa jamii, tumepambana na wala rushwa na wahujumu uchumi, tumewekeza katika miundombinu mikubwa, tumekataa pia baadhi ya nadharia za kimagharibi kwenye utendaji wetu na utungaji wetu wa sera za maendeleo” alisema Dkt. Abbasi.
Aidha, Dkt. Abbasi alitaja siri
nyingine kuwa ni azma ya kujitegemea, nidhamu katika matumizi,
kutekeleza miiko ya uongozi, kuwekeza kwenye miradi inayochechemsha
uchumi, maendeleo ya vitu na sekta binafsi yenye tija.
0 Comments