TAREHE YA MAFUNZO JKT KWA MUJIBU WA SHERIA HII HAPA…




📌NA DEVOTHA SONGORWA

MKUU wa Tawi la Utawala, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Kanali Julius Kadawi amewataka wahitimu wa kidato cha sita kwa mwaka 2020  waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kuripoti katika makambi walioyopangiwa kwa wakati ili kuanza mafunzo yanayotarajiwa kuanza nchini August mosi mwaka huu.

Kanali Kadawi ameyasema hayo jana jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa makao makuu ya jeshi hilo ambapo alisema kwamba vijana waliochaguliwa ni kutoka shule zote za Tanzania Bara.

Jeshi limewapangia makambi watakayokwenda kupata mafunzo na wanatakiwa kuripoti kuanzaia tarehe 24 hadi 27 mwezi huu kwa sababu mafunzo hayo yatafunguliwa tarehe mosi 2020  hivyo ni vyema wakazingatia muda uliowekwa
Kanali Kadawi.

Ameongeza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia vijana kujifunza uzalendo,umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa.

Akizungumzia wahitimu wenye ulemavu wa kuonekan akwa macho aliwataka kuripoti  katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo imewekewa miundombinu ya kuhudumia watu wenye mahitaji maalumu.

”Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma mkoani Mara, JKT Msange mkoani Tabora, JKT Ruvu mkoani Pwani, JKT Mpwapwa mkoani Dodoma, JKT Mafinga mkoani Iringa, ikiwemo JKT Mlale iliyopo mkoani Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba iliyopo mkoani Tanga.

Kambi zingine ni JKT Makuyuni mkoani Arusha , JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila Imkoani KIgoma , JKT Itanga  mkoani Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa mkoani Rukwa sambamba na JKT Nachingwea iliyopo mkoani Lindi, JKT Kibiti mkoani Pwani na Oljoro JKT iliyopo mkoani Arusha” Alizitaja Kanali huyo.

Kufuatia uwepo wa maambukizi ya virusi vya Corona nchini amesisitiz kwamba wamechukua tahadhali za kujingika kupata maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu kama zilizvyoelekezwa na serikali kupitia Wizara ya Afya  kwa kipindi chote vijana na watakapokuwa katika mafunzo yao.

Katika hatua nyingine Kanali Kadawi aliwataka waliochaguliwa kujiunga na mafunzo kutembelea tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz ili kufahamu orodha kamili ya waliochaguliwa, vifaa vinavyotakiwa na kambi walizopangiwa.

Post a Comment

0 Comments