TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 11.07.2020

Manchester United imejitayarisha kuingia kinyang'anyironi na Chelsea na Manchester City cha kumsaka mlinzi wa Leicester anayesemekana kuwa thamani yake ni pauni milioni 60 Ben Chilwell, 23. (Sun)

Kiungo wa kati wa Man City nyota Kevin de Bruyne, 29, amejitolea kusalia kwenye klabu yake hata kama marafuku ya kutoshiriki Ligi ya mabingwa kwa timu hiyo itadumishwa. (Mail)
Mlinzi Nicolas Otamendi, 32, na Oleksandr Zinchenko, 23, huenda wakatumika kwenye makubaliano ya mabadilishano na Napoli kwa mchezaji Kalidou Koulibaly, 29, wakati ambapo Manchester City inajitahidi kuwa wachezaji bora kuliko Manchester United na Liverpool. (Sun)

Manchester United inakaribia kukubaliana kiwango cha pesa na Fiorentina kwa winga wa Italia Federico Chiesa, 22. (Corriere Fiorentino via Star)

Winga wa Chelsea Willian amepewa ofa kubwa na Spurs wakati ambapo mkataba wa mchezaji huyo wa Brazil, 31, na Stamford Bridge unakaribia kumalizika mwisho wa msimu huu (Football Insider via Star)

Chelsea imeimarisha mipango yake ya kumtafuta mshambuliaji wa Ujerumani na Bayer Leverkusen Kai Havertz, 21, kwasababu mshambuliaji wao mwingereza Callum Hudson-Odoi, 19, hajafikia mchezo waliokuwa wanautarajia kutoka kwake. (90min)

Juventus imesemekana kwamba ilikuwa tayari kutoa ofa ambayo ingebadilisha kabisa maisha ya nyota Mason Greenwood mwaka jana ikiwa mchezaji huyo, 18, angeondoka Manchester United. (Athletic via Mirror)

Arsenal inakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan, Valencia na Real Betis katika mbio za kutaka kumsajili kiungo wa kati Dani Ceballos, 23, ikiwa inataka kutimiza makubaliano ya mkopo ya mchezaji huyo wa Uhispania kutoka Real Madrid kuwa ya kudumu. (Express)

Arsenal inakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan, Valencia na Real Betis katika mbio za kutaka kumsajili kiungo wa kati Dani Ceballos, 23, ikiwa inataka kutimiza makubaliano ya mkopo ya mchezaji huyo wa Uhispania kutoka Real Madrid kuwa ya kudumu. (Express)

Mlinzi Nicolas Otamendi, 32, na Oleksandr Zinchenko, 23, huenda wakatumika kwenye makubaliano ya mabadilishano na Napoli kwa mchezaji Kalidou Koulibaly, 29, wakati ambapo Manchester City inajitahidi kuwa wachezaji bora kuliko Manchester United na Liverpool. (Sun)

Barcelona imefikia makubaliano na Inter Milan na mshambuliaji wa Argentina Lautaro Martinez, 22, lakini makubaliano hayo yanategemea na ikiwa klabu ya Catalan inaweza kumuuza mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 28, ambaye msimu huu alikuwa Bayern Munich kwa mkopo. (ESPN)

BBC SWAHILI,

Post a Comment

0 Comments