NA HAMIDA RAMADHANI
Selukamba amekamatwa eneola Dodoma
Hoteli jijini hapa akitaka kuwapa rushwa wajumbe wa NEC,na wapiga kura
wake,huku Lusinde akikamatwa nyumbani kwake akigawa rushwa kwa wapiga kura
wake.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Takukuru mkoani
Dodoma Sosthenes Kibwengo alisema Takukuru Dodoma inaendelea na uchunguzi dhidi
ya watu hao,ilihali tayari awali wamekutwa na viashiria vya vitendo hivyo vya
rushwa ambavyo ni kinyume na sheria ya Takukuru.
Ni kweli tumewakamata wabunge hao na Takukuru inaendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuhakikisha ukweli wa suala hilo unajulikana.
Kibwengo.
Kibwengo amesema kwa upande wa Lusinde
inadawa kugawa fedha kwa wajumbe wa NEC CCM nyumbani kwake, huku mwenzake
amekutwa na kashfa hiyo katika maeneo ya Dodoma hoteli.
Amesema taarifa zilizosambaa kwenye
mitandao ya kijamii zilieleza kuwa mapema Julai 7,2020 kupitia kwa wasamaria wa
jimbo la Mtera, Livingston Lusinde (Kibajaji) amekamatwa na Takukuru na kuwekwa
chini ya ulinzi pamoja na kusitisha mkutano wake na wajumbe wa CCM.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa imekuwa ni
kawaida yake kuwaita wapiga kura wake na kuwaandalia chakula na baadaye
kuwapatia fedha kila ifikapo kipindi cha uchaguzi.
Kibwengo amesema julai 7,2020 Takukuru
ilipokea taarifa kutoka katika chanzo chake kuwa Mbunge huyo anagawa fedha kwa
wajumbe nyumbani kwake, ambapo baada ya maofisa wa taasisi hiyo kufika nyumbani
hapo waliwakuta wajumbe wa CCM takribani 20.
Amesema licha ya kuwakuta wajumbe hao
hawakukuta wakigawiwa fedha kama taarifa zilivyoeleza isipokuwa walikuwa
wameandaliwa chakula.
“Tuliwashikilia kwa muda hapo nyumbani
kwake kwa ajili ya kuwahoji, ambapo wao walijitetea kuwa wajumbe hao walifika
kumsalimia mtu amejifungua nyumbani hapo, lakini kama tunavyojua ukienda
kumsalimia aliyejifungua kuwezi kwenda bila zawadi lakini wao hawakwenda na
chochote,” alisema Kibwengo na kuongeza.
“Siwezi kuzungumza zaidi kwani bado
uchunguzi wetu unaendela dhidi ya tuhuma hizo kwa lengo la kupata ukweli zaidi,
lakini niwakumbushe wananchi wote kuwa rushwa haikubaliki na hatuwezi
kuwafumbia macho wanaojihusisha na vitendo vya kutoa au kupoke rushwa,”
amesema.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo
Livingston Lusinde akizungumzia tuhuma hizo amesema hajakamatwa na rushwa kama
ambavyo taarifa zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Hizo taarifa sio za kweli na mimi nimeziona kwenye mitandao ya kijamii, ni za uzushi tu.
Lusinde.
Mbunge huyo ambaye ameongoza nafasi hiyo
kwa awamu mbili mfufulizo kuanzia mwaka 2010 anatajwa kuwa ni miongoni mwa
watakaoomba ridhaa ya chama kugombea nafasi hiyo katika jimbo hilo.
Mbunge huyo anakuwa wa kwanza katika
mkoa wa Dodoma kuchunguzwa na Takukuru kutokana na kudaiwa kujihusisha na
rushwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Kwa upande wa Selukamba na naye amekutwa
na tuhuma kama hiyo hiyo ya kutaka kutoa rushwa.TAKUKURU imetoa wito kwa watia nia na wagombea kujihadhari na vitendo vya rushwa kwa kuwa taasisi hiyo imejipanga kukomesha vitendo vya rushwa katika chaguzi.
0 Comments