UNDP 'YAIPIGA TAFU' TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA






📌NA HAMIDA RAMADHANI
SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) limetoa msaada wa vifaa vya kielekteoniki zikiwemo  kompyuta na mashine za photocopy zenye gharama ya shilingi milioni160, kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala  Bora.

Akizungumza mara baada ya kupokea Vifaa hivyo mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ,amesema vifaa hivyo vitawasaidia kuendelea kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Aidha amesema kuwa UNDP sio mara ya kwanza kutoa msaada huo bali wamekuwa wakitoa msaada mara kwa mara kwa Tume ya haki za binadamu na utawala bora ikiwa ni sehemu ya kuiwezesha tume hiyo kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa UNDP na tunawaomba uisiwe mwisho kwani Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora bado inamahitaji mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yake.
 Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu.


Hata hivyo amesema vifaa hivyo vitawasidia kufanya kazi kwa ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku katika kuwahudumia wananchi.


Post a Comment

0 Comments