UWT KUPIGANIA WANAWAKE WALIOJITOSA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI



📌NA HAMIDA RAMADHANI
KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Taifa  (UWT) Queen Mlozi  amesema jumuiya hiyo itaendelea kuwapigania wanawake wote waliojitosa kugombea nafasi za uongozi kuhakikisha wanafikia adhma yao ya kupata nafasi hizo
Amesema UWT imejipanga kuhakikisha inawatendeahaki wanawake bila upendeleo na kuwataka waendelee kuchukua fomu za kupata uongozi.
 Mwalimu Queen ameyasema hayo wakati akitoa tamko la kuwahamasisha  wanawake nchini kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Wanawake wenye vigezo wa makabila yote na dini zote wachukue fomu za kugombea uongozi ilituweze kupata wawakilishi bila kujali au kuogopa chochote na UWT haitamuacha mwanamke aliyethubutu kwasababu uwezo tunao.     
Mwl.Queen Mlozi 
Akizungumzia mchakato wa kupata wawakilishi Katibu Mkuu huyo amesema wamejipanga kuanzia kwenye ngazi ya kata,wilaya,mkoa na taifa kuhakikisha haki inatumika pasipo upendeleo
Amesema uchaguzi wa mwaka huu utakuwa tofauti na miaka mingine kwani utakuwa wa wazi na kila kitu kitafanyika hadharani hakutakuwa na ujanja ujanja wala udanganyifu.
"kwa wale watakao pita kwenye chakato mbalimbali wa uchaguzi ni wahakikishie kuwa hakutakuwa na upendeleo wa aina yoyote, na tumejipanga vizuru  kuanzia ngazi ya chini hadi juu kuhakikisha haki inatumika, ilitupate viongoz wenye sifa ambao watakuwa viongozi,
"Vivyo hivyo uteuzi utakaofanyika baada ya uchukuaji wa fomu utakuwa uteuzi uliozingatia kanuni za uteuzi za wagombea   katika vyombo vya dora uliotolewa na CCM"ameeleza
Katibu mkuu huyo amewataka wanaohusika na utoaji fomu za kugombea uongozi kuacha mara moja kuongeza michango ambayo siyo ya lazima kwani inawea kukatisha tamaa watu ambao hawana kipato na wanataka uongozi.
alisema kila ngazi ya uongozi imeainishwa kikatiba gharama yake ya kuchukulia fomu.
"kwa udiwani fomu yake ni sh.10,000 na kwa ubunge ni sh.100,000 sitapenda kuona mtu anakuja kuchukua fomu halafu anaambia gharama za ziada mpeni fomu aende akaombe ridhaa kwa wananchi wake,
"Napenda kusisitiza kwa viongozi wanaotoa fomu za uongozi hatupendikuona mnaweka visingiti kwa watu ambao wanataka kuwatumikia wananchi mtu anapokuja kama kakidhi vigezo na masharti mpeni fomu mambo mengine yasiwepo"Amesisitiza .


Post a Comment

0 Comments