VING'ORA MARUFUKU DODOMA,MAGARI 27 YAKAMATWA



📌NA DOTTO KWILASA

Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma  limepiga marufuku magari ambayo sio ya viongozi na Ambulance  kupiga ving’ora na kuahidi kuendelea kuwasaka madareva wote wanaokiuka agizo hilo.

Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema Jeshi la Polisi limefanya msako na kufanikiwa kukamata magari 27 yaliyofungwa Ving’ora, vimulimuli,taa zenye mwanga mkali na zenye kubadilisha rangi ikiwa ni kutekeleza agizo lilotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Jeshi la Polis nchini IGP Simoni Siro.

Muroto amesema kuwa IGP alishatangaza kupiga marufuku gari yoyote ambayo siyo ya kiongozi wa Serikali, Ulinzi na Usalama, Zimamoto au Ambulance kutumia alama hizo kwenye gari zao.
Aidha Muroto amesema gari litakaloruhusiwa kutumia alama hizo ni ile ambayo  imepata kibali maalumu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani.

Magari hayo yaliyokamatwa yana kosa kisheria ya kwa kukiuka Kifungu 39(B) (1) (2) na kifungu cha 54(1)(2)(3)(4) na (5) cha Sheria ya Usalama Barabarani sura 168 ya mwaka 1973 na marejeo 2002
Kamanda Muroto.



Katika hatua nyingine,Kamanda Muroto amesema  wamefanikiwa  kuwakamata watuhumiwa watatu wakiwa na  gari aina ya Lori yenye namba za usajili T464 CGR ikiwa imepakia Drum 4 za nyaya za umeme aina ya ABC Conductor  zenye ukubwa mita 3200 ambazo zinatumiwa na Tanesco kusamabazia umeme.

Amesema wamefanikiwa kukamata gari hiyo inayodhaniwa imebeba mali ya wizi Julai 15 saa 10 jioni katika Kijiji cha Mbande Kata ya Sejeli Wilaya ya Kongwa katika barabara kuu ya Dodoma kuelekea Morogoro.

Baada ya kufanya uchunguzi wetu tulibaini watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha mzigo huo bila vibali wala risiti za manunuzi, na mbinu waliyotumia kuficha nyaya hizo chini ya mizigo ya bidhaa zingine za matumizi ya nyumbani
Kamanda Muroto .

Muroto amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Ramadhani Mussa (25) mkazi wa Mkuyuni Mwanza, Athuman Abbas (22) mkazi wa Bohari Mwanza na  Shafii Mussa (23) Mkazi wa Bohari Mwanza.

Kamanda Muroto amesisitiza watu kuacha kuhujumu Uchumi kwani Serikali inajitahidi kuweka miundo mbinu  kwa ajili ya kuwanufaisha Wananchi watu wanahujumu.

Post a Comment

0 Comments