VIRUSI VYA CORONA: FAMILIA YA AMITABH BACHCHAN YAKUTWA NA CORONA INDIA


Vizazi vitatu vya familia maarufu inayoshiriki katika filamu za Bollywood vimekutwa na virusi vya corona kulingana na maafisa katika jimbo la Maharashatra nchini India.
Matokeo siku ya Jumapili yalionesha kwamba muigizaji wa kike Aishwarya Rai Bachchan , ambaye aliwahi kushinda tuzo la malkia wa urembo duniani na mwanawe Aaradhya, mwenye umri wa miaka minane waliambukizwa virusi hivyo.
Mumewe Abhishek na baba mkwe Amitabh , wote waigizaji walipelekwa hospitalini siku ya Jumamosi wakiwa na virusi hivyo. Wote wawili walidaiwa kuwa na dalili chache za corona.
Abhishek Bachchan alichapsha ujumbe wa Twitter kwamba watasalia hospitalini hadi pale madaktari watakapoamua.
Aishwarya Bachchan mwenye urmi wa miaka 46 ni mojawapo wa waigizaji maarufu wa Bollywood nchini India na ughaibuni, wakishiriki katika filamu kadhaa za Bollywood na Hollywood.
Alishinda taji la malkia wa urembo duniani 1994 na ni balozi wa shirika la Umoja wa Mataifa UNAIDS .
Mwaka 2003 alikua raia wa kwanza wa India kuwa mwanachama wa jopo la Tamasha la filamu za Cannes . Aishwarya na mwanawe wanadaiwa kuwa hawana dalili.
Mumewe alituma ujumbe wa Twitter akisema kwamba wanajitenga nyumbani

BBC SWAHILI

Post a Comment

0 Comments