📌NA HAMIDA RAMADHANI
WAFANYAKAZI wa
Majumbani na Mahotelini wameiomba Serikali kuridhia na kupitisha Mkataba namba
189 ili uwasaidie kupata haki zao za msingi kama wafanyakazi wa kada zingine .
Hayo yamebainishwa leo
jijini Dodoma hapa katika warsha ya kikosi kazi cha kuendeleza mikakati ya
kuridhia Mkataba namba 189 iliyofamnyika katika ukumbi wa Maktaba .
Wakiongea na
Waandishi wa Habari wafanyakazi hao wa majumbani wamesema kuwa
kama Serikali itapitisha mkataba huo wafanyakazi wa ndani na mahotelini
watakuwa na nguvu ya kudai haki zao za msingi kama wafanyakazi wengine.
Akiongea kwa niaba ya
wafanyakazi wenzake Sarah Mwasandube amesema kuwa wafanyakazi wa ndani wamekuwa
wakidharaulika huku wakionekana kama watu maskini hali iliyopelekea hadi
kwenda kutumikishwa kazi hizo majumbani.
Amesema kutokana na
dhana hiyo waajiri wengi wamekuwa wakiwanyanyasa kwa kuwapiga,kuwabaka, kuwalawiti
na wengine kuwanyima mishahara yao.
Mkataba huu ukipitishwa wafanyakazi wa majumbani na mahotelini tutakuwa na nguvu katika kutetea haki zetu kwa nguvu kubwa.Sarah Mwasandube
Aidha,amesema kama mkataba huo utapitishwa pia utakuwa nyenzo imara kwa chama cha kutetea haki za wafanyakazi wa majumbani (CODAWU) kuwasaidia katika kuhakikisha wanapata haki zao.
Naye Dorisia Waziri ambaye
pia ni mfanyakazi wa ndani amesema kundi hilo linahitajika kupata haki zote
kama mfanyakazi mwengine ikiwemo bima ya afya,kuchangia mifuko ya hifadhi ya
jamii kwa ajili ya kujiwekea mafao yake ya uzeeni au kuacha kazi lakini hayo
yote yamekuwa tofauti kutokana na kutokuwepo kwa muongozo wa mkataba huo.
Kwa upande Mratibu wa
masuala ya Kijinsia kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Chiku Semfuko amesema
mkataba huo ni mzuri na umesimamia kazi zenye staha,ambapo mfanyakazi
anatakiwa afanye kazi sehemu salama.
Naye Michael Sabuni
kutoka Dawati la Jinsia la Jeashi la Polisi Wilaya ya Dodoma amesema kuwa
wamekuwa wakipokea kesi nyingi za wafanyakazi wa majumbani kwa kufanyiwa
ukatili ukiwemo hule wa kiuchumi .
Malalamiko mengi tunayoyapokea ni tabia za waajiri kuwakata wafanyakazi wa ndani makato mbalimbali ikiwemo yale ya hifadhi ya jamii lakini waajiri hawapeleki pesa hizo.Michael Sabuni
0 Comments