CRDB YATOA GAWIO KWA SERIKALI



Waziri wa Fedha, Dkt. Philip Mpango akipokea mfano wa hundi ya gawio la shilingi bilioni 9.3 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki yah CRDB, Dkt. Ally Laay (watatu kushoto) kutokana na uwekezaji wa Serikali ndani ya benki hiyo kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa DANIDA kwa kushirikiana na Serikali ya Denmark.

📌NA HAMIDA RAMADHANI

SERIKALI imepokea  Shilingi Billioni 9.3 kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni gawio la mwaka 2019 leo jijini Dodoma.

Akiongea  baada ya kupokea gawio hilo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Phillip Mpango amesema kuwa Benki ya CRDB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo katika Taifa.

Benki ya CRDB imekuwa ikiunga mkono na kutekeleza Mipango endelevu ya Taifa letu kila siku, Gawio ni sehemu moja wapo ya vyanzo vya Serikali
Dkt.Philip Mpango


Aidha Waziri Dkt.Mpango ametoa rai kwa tasisi zote za kifedha kusogeza zaidi huduma na kuhakikisha wanawafikia wananchi wa vijijini kwa kuwa hali iliyopo ya utoaji huduma za kibenki hairidhishi na kupelekea wananchi vijijini kuhifadhi fedha nyumbani

"Haiwezekani tupo Nchi ya Uchumi wa Kati alafu wananchi wetu bado wanahifadhi pesa chini ya godoro au kwenye mitungi ya maji nyumbani, hivyo sasa tasisi za Kifedha hakikisheni mnawafikia wananchi waliopo pembezoni," Amesema Waziri Mpango.

Kwa upande wa riba,Dkt. Mpango amesema riba za benki nchini bado sio rafiki kwa wakopaji na kuzitaka tasisi hizo za kifedha kuendelea kupunguza riba kwani imekuwa ni kikwazo kwa mtanzania wa hali ya chini.
 Niukweli usiopingika tasisi za Kifedha zimekuea na riba kubwa  huwa najiuliza sana kama tu Mimi Waziri siiwezi hiyo riba hii je vipi mwananchi wanaiweza nawaombeni endeleeni kuluona hili na tuwafikilie hawa wananchi wetu
Dkt.Philip Mpango

Awali akiongea kabla ya kukabidhi mfano wa hundi Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Msekela amesema CRDB ndio tasisi pekee ambayo imekuwa ikitoa asilimia 40 kwa ajili ya kilimo Tanzania.

Pia Msekela amesema Benki ya CRDB imekuwa ikiongoza kwa rasilimali  kwani ndio uwimara wa benk kwa kutoa wigo kwa watu bila kusahau kuongeza kwa Faida.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Benk Dk, Ally Laay amesema Benki hiyo ni ya watanzania hivyo wao wataendelea kuweka mikakati  yenye  ufanisi ili kupata fauda na kuendelea kutoa gawio kubwa kila mwaka kwa serikali.

Post a Comment

0 Comments