DIWANI KILIMANI ACHUKUA FOMU TAYARI KWA MPAMBANO



📌NA BARNABAS KISENGI 

DIWANI mteule kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Kilimani  Jijini Dodoma Neema Mwaluko leo  amechukuwa fomu ya kugombea udiwani wa kata hiyo

Awali akikabidhi fomu za Tume ya Uchaguzi, afisa mtendaji wa Kata ya Kilimani Fatuma Anti ambaye ndiye msimamizi wa Uchaguzi katika kata hiyo,amemwelekeza mgombea huyo kuhakikisha anazisoma fomu kwa umakini na kuzijaza kwa maelekezo yaliyo elekezwa katika fomu hizo kwa uadilifu na umakini. 

Mgombea hakikisha unafuata maelekezo yaliyopo kwenye fomu na pia hakikisha anarudisha fomu kwa muda alioelekezwa. 




Kwa upande wake Katibu wa CCM kata ya Kilimani Rotta Ndimbo akizungumza na wanachama waliomsindikiza diwani huyo amewataka wanachama wa CCM ndani ya kata hiyo kuvunja makundi.

Ndugu zangu tushirikiane,tuwe kitu kimoja ili kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika kata ya Kilimani.

Kwa upande wake diwani mteule Neema Mwaluko amewashukuru wanachama wa Kata hiyo kwa kumpatia ushirikiano kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na kuwapongeza kwa kumwamini tena kupeperusha bendera ya CCM



Aidha Mwaluko amekishukuru CCM kuanzia ngazi ya tawi Kata wilaya na mkoa kwa kuweza kumwamini baada ya kuongoza kura za maoni katika kata hiyo.

Post a Comment

0 Comments