LEAD FOUNDATION YAJIPANGA KUREJESHA UOTO WA ASILI DODOMA



📌NA RHODA SIMBA

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Lead Foundation limesema kutokana na mabadiliko ya tabia  nchi limejidhatiti  kurudisha uoto wa asili jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika maonesho ya Nane Nane kanda ya Kati,Mratibu wa Mradi Kinga Maji unaoendeshwa na shirika hilo wa Kinga Maji Bw. Samwel Msanjila lengo leo kuu ni kuona mkoa wa Dodoma unarudisha uoto wa asili.

Amesema kwa mikoa yenye ukame kama Dodoma mradi wa kingamaji ni muhimu kwa ajili ya kuvuna maji mengi kwa matumizi ya kilimo.

Na haya makinga maji unayoyaona tunayafanya mashambani na si kama yale yanayowekwa majumbaniMsanjila 
"Licha ya kutumika katika mashamba tunarudisha rutuba katika mashamba tunazuia mmomonyoko wa ardhi  na kurudisha uoto wa asili" Amasema. 

Amesema makinga maji hayo yanategeshwa mashambani katika msimu wa mvua ili kuweza kuvuna maji na moja kati ya mfano walioufanya wa makinga maji hayo ni katika kijiji cha Pemba Moto kilichopo  wilayani kongwa.

 Shirika la Lead Foundation lilianzishwa miaka kumi (10) iliyopita na Askofu  Mstaafu wa kanisa la Anglican Mpwapwa Simoni Chiwanga likiwa na lengo la kusimamia mafunzo ya usimamizi wa mazingira,mafunzo ya uongozi bora na miradi midogo ya maendeleo ya jamii.


Post a Comment

0 Comments