EWURA YATOA SABABU KUADIMIKA KWA MAFUTA, MAFUTA BEI JUU


A


 ðŸ“ŒHAMIDA RAMADHANI

MAMLAKA  ya Udhibiti wa Nishati na Maji Nchini (EWURA) imetoa sababau ya kuadimika kwa mafuta kuwa ni kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya Petroli .

Aidha kuanzia Juni 2020 matumizi ya petroli yaliongezeka kufikia lita mil.3.683 kwa siku na Julai 2020 matumizi yaliongezeka  zaidi kufikia lita mil.4.425 kwa siku ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 21.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dodoma, Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa  Ewura, Titus Kaguo amesema pia bei mpya za mafuta zitaanza kutumika kesho Agast 5 katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha pamoja na ongezeko hilo amesema akiba ya mafuta iliyokuwepo katika magahala iliendelea kutosheleza mahitaji ya nchi

Kuanzia Julai 29 hadi 31 Agosti 2020 kuna jumla ya meli sita za petrol zinazotegemewa kupokelewa ambapo kati ya hizo meli tatu zimeshawasili nchini zikiwa na jumla ya lita mil. 89.564 kwaajili ya soko la ndani na zitatosheleza matumizi ya zaidi ya siku 18
Titus Kaguo.

Pia amesema kuwa meli nyingine tatu zitawasili kati ya Agosti 17 na 31 mwaka huu zikiwa na takribani lita mil.100.075 zitakazo tosheleza mahitaji ya nchi kwa zaidi ya siku 22.

Kwa upande wa mafuta ya Diesel  Kagua alisema kuwa yapo yakutosha na meli tatu za mafuta hayo zenye jumla ya lita mil.193.391 zinategemewa  kuwasili nchini Agosti 2020 ambapo mafuta hayo yatatosheleza mahitaji ya dizeli kwa zaidi ya siku 30.

“Ili kuwa na utoshelevu wa mafuta nchini,kuanzia Septemba 2020 Ewura imeongeza makadirio ya matumizi ya mafuta kwa siku kuwa lita mil.4.812 kwa petrol na lita mil.6.082 kwa dizeli.

“Wakala wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja (PBPA)atatumia makadirio haya wakati wa kuagiza mafuta,”amesema.

Amesema Petroli itaongezeka kwa shilingi 139 kwa lita  kwenye toleo lilotoka Julai ambapo itakuwa  imeongeza kwa asilimia 8.22 huku kwa upande wa  Diesel ikiongezeka kwa shilingi 69 sawa na asilimia 4

Tunakuja na bei mpya kuanzia Jumatano kesho Petroli imeongezeka  kwa shilingi 139 kwa lita  kwenye toleo lilotoka Julai kwahiyo imeongeza kwa asilimia 8.22 huku Diesel ikiongezeka kwa shilingi 69 sawa na asilimia 4 
Titus Kaguo.

Amesema kwa Dar es salaam  bei ya zamani kwa Petroli ilikuwa sh.1693 sasa itauzwa kwa  sh.1832.
Amesema Mkoa wa Tanga bei imeongezeka kwa shilingi 214 sawa na asilimia 12.94 huku Diesel ikiongezeka kwa shilingi 85 sawa asilimia 5.02.

Amesema Diseli awali ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 1693 ambapo sasa itauzwa kwa shilingi 1778 na Petroli awali ilikuwa shilingi 1654 sasa itauzwa kwa shilingi 1868.

Amesema kwa Mkoa wa Mtwara Petroli imeongezeka kwa shilingi 263 sawa na asilimia 12.29 huku Diesel ikiongezeka shilingi 68 sawa na asilimia 3.95.

Amesema kwa Mkoa wa Mtwara Petroli itauzwa kwa shilingi 1875 ambapo awali ilikuwa ni shilingi 1612 huku Diesel ikiuzwa kwa shilingi 1799 ambapo awali ilikuwa ni shilingi 1731.


Meneja Biashara wa Ewura,Kemilembe Kafanabo

Akizungumzia sababu za bei kuwa tofauti katika Mikoa ya Tanga na Mtwara,Meneja Biashara wa Ewura,Kemilembe Kafanabo amesema ni kutokana na bei kutofautiana katika soko la dunia.

“Kwa Mkoa wa Tanga  mafuta mara ya mwisho yalipokelewa katika Bandari ya Tanga mwezi wa nne  mafuta yale yalikuwa na bei ya soko la dunia ya  mwezi wa tatu na sote tunafahamu kwamba bei za soko la dunia zilianza kushuka kwa kiwango kikubwa kuanzia mwezi wa nne.

“Kwa hiyo bei za kutokea bandari ya Tanga zimedumua kuanzia kipindi kile hadi leo ndio sababu tunaona kuna ongezeko kubwa katika badari hiyo.

“Kwa Mtwara yalipokelewa  kwa vipindi tofauti kuanzia mwezi wa tatu hivyo kutokana na utofauti mzigo unakuwa na bei tofauti kutokana na kipindi ambacho kimepokelewa,”amesema Kafanabo

Akizungumzia upande wa usambazaji wa mafuta nchini Kaguo amesema kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya petrol iliyojitokeza mwishoni mwa Julai 2020 imechangiwa na kuchelewa kwa meli moja iliyokuwa ifike nchini kati ya julai 22 na 24 mwaka 2020 na badala yake ikawasili julai 29 mwaka huu.

Kuchelewa kwa meli hii kulitokana na changamoto zilizokuwepo katika ‘refinery’ yalikotokea mafuta hayo na upepo wa Monsoon huko baharini uliyofanya meli kusafiri kwa kasi ndogo

Amesema kutokana na kuchelewa kwa meli hiyo kwa takribani siku 7,kuna uhaba kidogo uliojitokeza katika maeneo machache,ambapo  Ewura ilifanya mawasiliano na kampuni za mafuta kuhakikisha mafuta yanapatikana maeneo yote.

Aidha amesema kuwa usambazaji wa mafuta kwa sasa nchini niwakuridhisha na maeneo yote yana mafuta ya kutosha isipokuwa maeneo machache.

“Hali ya upatikanaji wa mafuta  Kanda zilizo chini ya Ewura ni pamoja na Kanda ya Mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es salaam,Mtwara,Lindi,Pwani na Morogoro ambapo mafuta yanapatikana bila matatizo,”amesema.


Vilevile Kanda ya Kaskazini inayojumuisha mikoa ya Tanga,Arusha,Kilimanjaro na Manyara mafuta yanapatikana bila matatizo,na Kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma,Tabora,Singida na Iringa pia yanapatikana bila matatizo.

Kanda ya Nyanda za juu kusini inayojumuisha mikoa ya Ruvuma,Njombe,Mbeya,Songwe,Rukwa na Katavi ambapo mafuta yanapatikana isipokuwa kuna uhaba ulijitokeza katika Mji wa Mpanda mkoani Katavi na hata hivyo kuna lita 37,000 ambazo zimeanza kuuzwa  na kuna lita 100,000 ziko njiani zikitegemewa kuwasili leo jioni.
Titus Kaguo.

Hata hivyo amesema kuwa Kanda  ya Ziwa inayohusisha mikoa ya Mwanza,Mara,Simiyu,Kagera na Kigoma mafuta yanapatikana isipokuwa kuna uhaba umejitokeza katika Wilaya za Bunda na Musoma mkoani Mara.

“Hii inatokana na kuchelewa kuondoka kwa magari ya mafuta kutoka Dar es salaam kuelekea maeneo hayo hasa kwa kuzingatia kuwa kulikuwa na siku tatu ambazo siyo za kazitangui ijumaa ya julai 31 mwaka huu.

“Mafuta yamekwishapakiwa na yako njiani kuelekea katika maeneo husika ikitegemewa mafuta hayo yatafika kati ya leo na kesho,”amesema.

Post a Comment

0 Comments