IKUPA AWATAKA WAKULIMA KUZINGATIA USHAURI UNAOTOLEWA NA WATAALAM


NA HAMIDA RAMADHANI


NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye Ulemavu Stella Ikupa amesema kuwa Tanzania ni Nchi iliyojaliwa ardhi nzuri yenye rutuba hivyo Wakulima wazingatie ushauri unaotolewa na wataalamu wa kilimo kwani kilimo kinalipa.

Hayo yamesemwa leo jijini hapa katika siku ya kilele  Cha maadhimisho ya Maonesho ya wakulima na wafugaji Nanenane kanda ya Kati kwenye viwanja vya Nzuguni Dodoma.

Ikupa amesema asilimia 70 ya watanzania wamejikita katika shughuli za kilimo,Ufugaji na Uvuvi na hivyo kwakuzingatia ushauri wa wataalamu sekta hizo zinaweza kuwakomboa watanzania.

KWA UPANDE WA UFUGAJI 

Ikupa amesema kuwa Ufugaj wetu sio wenye tija wafugaji wanafuga bora kufuga na sio kufuga kwa malengo na kuwataka wafugaji kubadilika kufuga kisasa Ng' ombe kidogo faida kubwa na kuachana na habari ya kuwa na mlundikano wa mifugo isiyoleta faida.


Na hii inasaidia Sana kuondoa migogoro ya ardhi iliyopo Kati ya wakulima na wafugaji kwani wakulima wataweza kulima na wafugaji watakuwa na uwezo wa kumiliki eneo la malisho kwa mifugo yao bila migongano
Stella Ikupa

Aidha amesema  maendeleo yanaletwa na kiongozi bora hivyo katika kuelekea kipindi Cha uchaguzi tudumishe Amani,utulivu na uzalendo kwani sifa ya mtanzania ni kuwa mzalendo

Amesema hata haya maendeleo mengi na bora tunayoyaona ni kutokana na kuwa na kiongozi bora na mwenye Nia thabiti ya kuwafikisha mbali watanzania wanyonge.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk,Rehema Nchimbi amesema amemshukuru Rais John Magufuli kwa kuifanya Dodoma kuwa jiji kwani huko nyuma kanda ya Kati haikuwa kama ilivyo Sasa na wananchi wake walikuwa wanyonge kwa kuitwa mikoa yenye shida.

"Tumeweza kuona Mikoa ya  Dodoma Singida sio masikini Wala sio kame kwani shida iliyokuwepo nikuto utumia ushauri uliokuwakuitolewa na watalamu ,"amesema Dk,Nchimbi.


Post a Comment

0 Comments