JAFO AIPA 'TANO' CiC KWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI YA USOMAJI



Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) akimkabidhi cheti cha umahiri wa ufundishaji darasa la elimu ya awali Mwalimu wa darasa la awali  Monica Kibena kutoka shule ya msingi madizini wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.

📌NA JOYCE KASIKI



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais ,Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amelipongeza Shirika linalosaidia watoto wanaopitia katika changamoto  mbalimbali (CiC) kwa kuelimisha walimu namna ya kuwa na darasa la elimu ya awali katika mradi wake wa Watoto wetu tunu yetu.

Jafo ametoa pongezi hizo hivi karibuni jijini Dodoma  katika maadhimisho ya siku ya Tamisemi Idara ya Elimu alipotembelea banda la  CiC na kujionea darasa la awali la mfano lililosheheni zana rahisi za kufundishia zinazomwezesha mwanafunzi wa darasa hilo kuelewa kwa haraka zaidi lakini pia kumwezesha mwalimu kulimudu darasa hata likiwa na wanafunzi wengi.

Katika siku hiyo baadhi ya walimu wanaofundisha madarasa ya awali walitunukiwa vyeti kwa umahiri wa kufundisha madarasa hayo miongoni mwao akiwa ni Mwalimu Monica Kibena kutoka shule ya msingi Madizini wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro,ambaye ni mmoja wa walimu waliopo katika mradi wa Watoto Wetu Tunu Yetu.

Akimuelezea Waziri Jafo umuhimu wa kuwa na darasa hilo Mwalimu wa darasa la awali katika shule ya msingi Madizini wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Monica Kibena amesema,darasa la awali linapaswa kuwa na kona za kujifunzia na lenye zana za somo husika kwani watoto wa darasa hilo hujifunza zaidi kwa vitendo.
Mwalimu Monica Kibena akimuelezea Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi ) Selemani Jafo alipotembelea banda la CiC na kujinea darasa la mfano kwa wanafunzi wa darasa la awali.

Hili ni darasa la awali,na kwa kutumia zana zinazopatikana katika mazingira yetu ,madarasa kama haya yanaweza kuwepo nchi nzima.
Monica Kibena

Shirika la CiC linatekeleza mradi wa Watoto Wetu tunu Yetu katika mikoa ya Mwanza,Morogoro na Dodoma ambapo kwa mkoa wa Dodoma mradi umeanza mapema mwaka huu na unatekelezwa katika wilaya za Kongwa na Chamwino.

Aidha Shirika la CiC ,linafanya kazi na Shirikisho la Vyama vya waandishi wa Habari nchini (UTPC) kupitia klabu za waandishi wa Habari kuhusu malezi na makuzi ya awali ya mtoto.

Mfano wa darasa la awali ambalo limeheheni 
picha za michoro na za rahisi zinazopatika katika mazingira yetu.


Post a Comment

0 Comments