"JAMII LAZIMA IWAJIBIKE SIO KUACHIA SERIKALI PEKE YAKE"-UTOUH


📌NA HAMIDA RAMADHANI
IMEELEZWA kuwa suala ya uwajibikaji sio la Serikali pekee bali ni Jamii kwa ujumla kwa kuhakikisha jamii inafahamu masuala mbalimbali yanayoendelea Nchini katika nyanja tofauti.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Wajibu na aliekuwa CAG mstaafu Ludovick Utouh wakati akifungua Mkutano
Wa Uzinduzi wa Ripoti ya uwajibikaji kwa Mwaka 2018/19 uliofanyika leo Jijini Dodoma na kushirikisha Taasisi mbalimbali.
Utouh amesema kuwa kupitia Uzinduzi Wa Ripoti hiyo ambayo ni ya Nne inalenga kurahisisha taarifa za CAG kwa wananchi kueleweka vyema ikiwa pamoja na kuimarisha uwajibikaji na Utawala bora katika kukuza Uchumi wa Nchi.
Meneja Fedha Na Utawala Wajibu Jackson Mmary amesema miongoni mwa mafanikio yaliopatikana katika Ripoti mbalimbali zinazozinduliwa na taasisi ya wajibu kupitia taarifa za CGA ni kuleta maendeleo kwenye jamii na mchango mkubwa pamoja na waandishi wa Habari.
Katika Uzinduzi huo umeenda sambamba na Mjadala wa maoni na mapendekezo juu Changamoto mbalimbali katika suala la uwajibikaji na utawala bora ambapo mwakilishi wa Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali Salihina Mkumbo amesema kuwa ofisi ya CAG itaendelea kushirikia na tasisi ya Wajibu huku akipongeza juhudi zilizofanya na Taasisi ya hiyo.

Post a Comment

0 Comments