JPM KUKABIDHI UENYEKITI SADC:UGAIDI,UMASKINI NA MIGOGORO BADO 'PASUA KICHWA'





📌NA .FAUSTINE GIMU GALAFONI

Mkutano wa 40 wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini ya Afrika (SADC) umefanyika   leo  Agosti 17,2020 Chamwino jijini Dodoma kwa njia ya Video  ambapo  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa jumuiya  hiyo Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  amekabidhi  uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Msumbiji  Mhe. Filipe Nyusi.

Katika mkutano huo Rais John Magufuli anatarajiwa kukabidhi jukumu la uenyekiti wa SADC kwa Rais wa Msumbiji Philipe Nyusi.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya Mtandao,Mwenyekiti huyo mstaafu wa SADC,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli amesema katika mwaka mmoja wa Uongozi wake katika Jumuiya hiyo  kuna mafanikio mbalimbali ikiwemo usimamizi wa ajenda za Maendeleo za SADC pamoja na kuridhiwa kwa lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa Lugha nne za SADC.

Aidha,Dkt.Magufuli amesema Jumuiya ya SADC bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo umasikini,migogoro ,ugaidi  pamoja na magonjwa hivyo kuna umuhimu wa kushirikiana.



Katibu Mkuu wa SADC Dkt.Stergomena Laurance Tax amesema baada ya kuendelea mtengamano wa SADC bado kuna kazi kubwa katika kuhamasisha ujenzi wa viwanda katika ukuaji wa kiuchumi huku Mwenyekiti mpya wa SADC   Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi   akitoa pongezi kwa kupewa heshima hiyo ya uenyekiti.



Ikumbukwe kuwa Rais Magufuli alikabidhiwa uenyekiti wa SADC Agosti 17,2019 kutoka kwa Rais wa Namibia Dkt.Hage Geingob alioutumikia wadhfa huo kwa Mwaka mmoja  na takriban nchi 16 zinaunda jumuiya hiyo ya SADC ambazo ni Tanzania,Angola,Botswana,Kongo,Lesotho,Madagascar,Malawi,Morisi,Msumbiji,Namibia,Afrika kusini,Uswazi,Shelisheli,,Zambia na Zimbabwe ambapo jumiya hiyo pia imetimiza miaka 40 tangu ianzishwe mwaka 1980.

Pia idadi ya  nchi wanachama imengezeka  kutoka nchi 9 waanzilishi hadi kufikia nchi 16 hivi sasa na idadi ya watu ikiongezeka  kutoka milioni 60 hadi milioni 350 hivi sasa na Kaulimbiu ya mkutano wa SADC 2020  ni;’Miaka 40 ya kuimarisha amani na usalama, kukuza maendeleo na kuhimili changamoto zinazoikabili dunia’

Post a Comment

0 Comments