KITABU CHA HISTORIA YA RAIS MAGUFULI KUZINDULIWA DODOMA



📌NA HAMIDA RAMADHANI

WAZIRI  wa Mambo ya Nje ya  Nchi Profesa Palamagamba Kabudi anatarajiwa kuwa mgeni  rasmi  katika uzinduzi wa kitabu cha historia  ya Rais John Magufuli.

Akiongea na waandishi  wa habari leo Jijini  Dodoma  Mwandishi  wa kitabu hicho Mathias Joseph Kabadi amesema kitabu  hicho  kinaeleza maisha  binafsi ya Rais Magufuli kuanzia utoto , Siasa, alivyaanza kufanya kazi mpaka sasa alipo.

 Uzinduzi wa kitabu hicho  utafanyika tarehe 5 August mwaka huu katika viwanja vya Nyerere Square jijini  hapa.

Kilichonisukuma kuandika historia hii ni kutokana na uwajibikaji wake ,pili kulikuwepo na changamoto juu ya uraia wake zikidai kuwa yeye si mtanzania hivyo kitabu hiki kitasaidia Wananchi kumjua vizuri Rais Magufuli
Mathias Joseph Kabadi

Amesema  kitabu hicho kitauzwa kwa bei ya shilingi 5000 ili kuwezesha kila Mtanzania kusoma kitabu hicho na baada ya uzinduzi kitabu hicho kitasambazwa nchi nzima ili Watanzania wakisome na kumfahamu Rais Magufuli..


Post a Comment

0 Comments