LEAD FOUNDATION YAENDELEA NA MPANGO MKAKATI WA KUKUFUA MITI KWA NJIA YAKISIKI HAI




📌NA HAMIDA RAMADHANI

KATIKA juhudi za kuifanya Dodoma kuwa ya kijani Tasisi isiyo ya kiserikali ya Lead Foundation inaendelea na mpango mkakati wa kukufua miti iliyokufa kupitia mradi uitwao Kisiki Hai.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo katika  banda lao la Maonesho katika viwanja vya nane nane ,Mratibu  wa mradi huo Josia Ngamagila amesema mradi wa Kisiki hai umekuwa ni moja kati ya mradi  kombozi wa ardhi iliyochakaa .

 Ameeleza kuwa kisiki hai ni mti hai ardhini ambapo kama tungeweza kuona chini ya ardhi tungetambua kuwa Kuna mti mkubwa kama ule tunaouona juu ya ardhi.

 Aidha ameelezea njia ya kutunza kisiki hai ni pamoja na kutunza maotea ya miti inayochipua kutokana na kisiki hai au mbegu za miti zikizodondoshwa ardhini na vinyesi vya wanyama au ndege.

" Njia hii ya kisiki hai imeitwa mkombozi wa mazingira hasa katika maeneo kame kwasababu kuu nne ambazo ni gharama nafuu,endelevu,rahisi kwa mtu yoyote,na imekua ikileta matokeo kwa muda mfupi"amesema Ngamagila.

Na kuongeza kusema kwamba kwa kutumia njia ya kisiki hai ambayo ina hatua nne inasaidia kuweza kurejesha shamba la mtu kuwa lenye rutuba tena
Ngamagila.

FAIDA YA KUTUMIA KISIKI HAI.

Ngamagila amesema kuwa na miti mingi shambani Kuna faida nyingi sana kwani miti haizuii tu mmomonyoko wa udongo na kuongeza rutuba ardhini,bali inachangia katika vitu vingi kama chakula kwaajili ya lishe bora na dawa za matibabu na matawi madogo kwaajili ya kuni majumbani.

 Pia amesema inachangia katika malisho na vivuli kwaajili ya mifugo na katika kuonesha mipaka katika mashamba ya wananchi.

Tunaelewa kuwa watu wanaogopa kuwa na miti mashambani kwa imani ya kwamba itapunguza kiwango cha mavuno mashambani jambo ambalo si la kweli kwani ushahidi na vipimo vinaonesha kuwa mavuno yanaongezeka unapotekeleza njia ya Kisiki hai
Ngamagila.

Ameongeza " kwa kutunza miti,udongo utakua na majani ya miti ambayo baada ya muda yanakua mbolea na inapunguza joto ardhini na kuleta mvua" amesema

Mpka sasa miti zaidi ya million 5.6 imestawishwa kwa njia ya Kisiki Hai katika Mkoa was Dodoma wamewafikia wakulima zaidi ya 200 na Kaya Laki 2.

Post a Comment

1 Comments

  1. Great and amazing, I think government should join and extend the project national wide not only in Dodoma.
    Big up LeadFoundation! Great Mr. Josy for the good job keep it up!

    ReplyDelete