MAFUNZO:JAMII,WAANDISHI WATAKIWA KUENDELEA KUJIKINGA

Dkt.Francis Lutalala akisisitiza matumizi ya vitakasa mikono

JAMII imetakiwa kuendelea kutumia mbinu zilizotumika kupambana na ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona ambao bado unaendelea kusumbua baadhi ya nchi duniani.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika mafunzo ya siku moja ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Covid 19 yaliyofanyika mwishoni mwa wiki, Dkt.Francis Lutalala akiwasilisha mada kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa Dodoma amesema licha ya maambukizi ya ugonjwa huo kuwa chini hapa nchini,ni vyema wananchi wakaendelea kufuata ushauri wa watalaamu wa afya na iwe sehemu ya maisha yao.

Dkt.Lutalala amesema tahadhari zilizotumika kujinga na ugonjwa wa Covid19 zinapaswa kuwa endelevu kwa vile zinasaidia kujinga kwa magonjwa mengine ya mlipuko katika jamii ikiwemo kipindupindu .

Katika kupambana na corona tulisisitizwa sana usafi,unaponawa mikono yako kwa maji na sabuni unakuwa salama zaidi hata unapoenda kula chakula,hivyo inakuwa sehemu ya kujikinga na magonjwa yatokanayo na uchafu hivyo tuendelee na maisha hayo 

Dkt.Lutalala

Dkt.Francis Lutalala akitoa somo juu ya namna bora ya kuvaa barakoa

Pia Dkt. Lutalala ametoa wito kwa Waandishi wa Habari nchini kuendelea kujilinda kwa vile kazi yao inawakutanisha na watu wengi wa aina mbalimbali hivyo njia pekee ya kubaki salama ni kufuata taratibu zililozowekwa na wataalamu wa afya kabla na baada ya mikusanyiko.

Amesema kwa mazingira ya kazi ya uandishi hapa nchini,waandishi wanatakiwa kuchukua tahadhali kwa kuzingatia miongozo hiyo ili kutimiza majukumu yao huku nao wakibaki salama na familia zao .

Tujitahidi kuendelea kunawa mikono au kutumia vitakasa mikono (sanitaiza) mara kwa mara,tunashikana mikono na watu wengi na wa aina mbalimbali kwa siku pia hata kuvaa barakoa ikibidi,itatusaidia kubaki salama.

 Dkt.Lutalala

Dkt.Lutalala akimkabidhi Mwanachama wa CPC Bahati Msanjila vipeperushi
vyenye jumbe mbalimbali za kujinga na ugonjwa wa COVID19

Licha ya kujilinda,Dkt.Lutalala amewataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao  kuelimisha jamii kuendelea kuchukua tahadhali katika kuendelea kukabiliana na magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Amesema kama jamii itaendelea kufanya yale yaliyofanywa katika mapambano dhidi ya corona ikiwemo kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu Tanzania itafanikiwa kutokomeza magonjwa ya mlipuko yakiwemo yanayoambukizwa kwa njia ya hewa.

 
Dkt.Lutalala akionesha mfano wa kunawa maji na sabuni,aliyesimama
pembeni yake ni Mwenyekiti wa CPC,Mussa Yusuph.


Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dodoma (CPC) na Umoja wa Vilabu Vya Habari nchini (UTPC),Mwandishi mkongwe Shija Nour ambaye pia ni Mhariri wa gazeti la Mwananchi amewasilisha mada ya namna ya kuandika Habari za Magonjwa ya Mlipuko kwa waandishi wanachama wa Central Press Club.
Shija amewataka waandishi kutotumia maneno ambayo yataongeza hofu katika jamii wakati wa kuripoti taarifa Habari za milipo.

Wakati wa kuandika Habari magonjwa ya mlipuko ni lazima tuwe na uchaguzi wa maneno sahihi ili kuepusha kuwachanganya wasomaji wetu na kueneza hofu kwa wananchi.

Shija Nour

 
Mwandishi mkongwe Shija Nour akiwasilisha mada


Pia nguli huyo amewata waandishi wa habari kushirikiana kwa karibu na wataalamu wa sekta ya afya ili kupata taarifa na misamiati sahihi ya magonjwa ili kupeleka elimu sahihi kwa wasomaji.

Kwa upande wa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo,Dotto Kwilasa na Barnabas Kisengi wamesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo mkubwa wa kujinga magonjwa ya mlipuko wakati wa kitimiza majukumu yao ya habari pamoja na kupata uelewa wa namna bora ya kuhabarisha umma kuhusu magonjwa ya mlipuko.

Mwandishi wa gazeti la Mwanachi Rachel Chibwete
akisisitiza jambo wakati wa mafunzo

Mwandishi wa gazeti la Zanzibar Leo Saida Khamis
akifafanua jambo wakati wa mafunzo.

Mwandishi wa Star Tv -Dodoma Blaya Moses 
akifafanua jambo wakati wa mafunzo.




Post a Comment

0 Comments