'MBIVU NA MBICHI 'ZA UBUNGE CCM 2020



📌NA FAUSTINE GIMU GALAFONE

Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Agosti 20, 2020 imetangaza majina ya wateule watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, 2020

Akitangaza  majina ya wagombea  makao makuu ya CCM jijini Dodoma,katibu Mwenezi wa chama hicho Humphrey Polepole amesema waliopitishwa kugombea Ubunge katika Mkoa wa Shinyanga kwenye uchaguzi Mkuu 2020 ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini ,  Patrobas Katambi ambapo atagombea  jimbo la Shinyanga Mjini.

Wengine ni  Boniface Butondo  jimbo la Kishapu, Idd Kassim jimbo la Msalala,Elias Kwandikwa jimbo la  Ushetu,Jumanne Kishimba jimbo la Kahama Mjini na Ahmed Salum  Jimbo la  Solwa.
Katika mkoa wa Dar es Salaam waliopitishwa kugombea Ubunge kupitia chama hiko ni pamoja na Aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile katika jimbo la Kigamboni, Dkt. Josephat Gwajima jimbo la Kawe, Abdallah Chaurembo jimbo la Mbagala, Dorothy Kilave jimbo la Temeke.

Dkt. Kitila Mkumbo jimbo la Ubungo, Issa Jumanne Mtemvu jimbo la Kibamba, Jerry Slaa jimbo la Ukonga, Bona Kalua jimbo la Segerea, Abbad Tarimba jimbo la Kinondoni pamoja na Mussa Zungu jimbo la Ilala.
Chama cha Mapinduzi[CCM],kimetangaza wagombea watakaokiwakilisha Chama hicho Kutetea kiti cha Ubunge katika Majimbo yote 264 hapa nchini Tanzania.

Post a Comment

0 Comments