MFUMUKO WA BEI: BIDHAA ZA VYAKULA KINARA


📌NA RHODA SIMBA.

MFUMUKO  wa bei  wa Taifa Kwa mwaka ulioishia julai  2020 umeongezeka hadi kufikia asilimia 3.3 kutoka  asilimia 3.2 kwa mwaka ulioishia Juni 2020.

 Akizungumza na waandishi wa habari  leo  kaimu Mkurugenzi  wa sensa  na takwimu  za jamii  Luth Minja amesema kuongezeka kwa bei  kwa mwaka unaoishia  julai   2020 kumechangiwa  na kuongezeka  kwa bei za baadhi ya  vyakula  na bidhaa zisizo za vyakula  Kwa  kipindi  kilichoishia mwezi  julai 2020 zikilinganishwa  na  bei  za mwezi  julai 2019.

Baadhi  ya bidhaa za vyakula zilizoongezeka  bei kwa mwezi Julai 2020 zikilinganishwa  na bei  za mwezi  Julai 2019 ni pamoja  na unga wa  mahindi  kwa asilimia 7.9, mtama  kwa asilimia  4.8 unga  wa muhogo  kwa asilimia 3.0 dagaa  kwa  asilimia 3.8 matunda  kwa asilimia  4.0 na mboga mboga  kwa asilimia  9.6 Minja.
"Kwa upande wa bidhaa zilizochukuliwa za vyakula  zilizoongezeka  bei  kwa mwezi  julai 2020 zikilinganishwa na bei  ,za mwezi  julai 2019 ni pamoja na  mavazi  kwa asilimia  2.8 gesi ya kupikia  kwa asilimia 5.9 samani kwa  asilimia 2.7 gharama 2.7 gharama za utengenezaji  na ukarabati  wa nyumba  kwa asilimia  6.2 na mkaa  kwa asilimia 11.6" amesema

Amesema mfumko wa  bei wa bidhaa za vyakula  na vinywaji  baridi  kwa mwezi  julai 2020 umebaki  kuwa asilimia  3.8 kama ilivyokuwa  kwa  mwaka ulioishia  mwezi juni 2020.

Kwa upande wa  nchi za Afrika  mashariki  Kwa mwezi  ulioishia Julai 2020  nchini Kenya  mfumuko  wa bei  umepungua hadi kufikia  asilimia 4.36 kutoka  asilimia  4.59 Kwa mwaka  ulioishia  mwezi  juni  2020.

Kwa upande wa Uganda Mfumuko  wa bei  kwa mwaka ulioishia  mwezi  julai 2020 umeongezeka hadi  asilimia  4.7 kutoka  asilimia  4.1 kwa mwaka ulioishia  mwezi juni 2020
Minja.

Hata hivyo mfumko  wa bei  wa  taifa  unapima  kiwango cha  kasi  ya mabadiliko  ya bei  za  bidhaa  na huduma  zote zinazotumiwa  na kaya binafsi nchini .

Post a Comment

0 Comments