MH.MAVUNDE-"MTU APEWE SIFA ZAKE AKIWA HAI"



📌NA HAMIDA RAMADHANI
WATANZANIA wametakiwa kuacha tabia ya kumsifia mtu pale anapokufa na badala yake wametakiwa kujenga mazoea  au tamaduni ya kumsifia mtu anapokua hai ili aweze kusikia sifa zake.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi Vijana Ajira na Watu wenye Ulemavu Antony Mavunde katika uzinduzi wa Kitabu chenye historia ya maisha ya Rais wa Tanzania  Dk.John Pombe  Magufuli .

Mavunde amesema yapo mengi Rais huyo wa awamu ya tano ameyafanya hivyo ni vyema yakaandikwa ili vizazi na vizazi waweze kuja kufahamu Mambo mengi mazuri yaliyofanywa na kiongozi huyo.

"Nikupongeze sana mwandishi wa kitabu hiki Mathias Kabadi umefanya vizuri kwa kuandika historia ya Rais wetu umeweza kupita katika maeneo mbalimbali kukusanya taarifa na umeeleza maisha,elimu,utawala na ujuzi wake hakika umewafanya watanzania kumjua Zaidi kupitia Kitabu hiki,"amesema Naibu Waziri huyo Mavunde.

Hii nifursa ya kipekee kumpata kiongozi kama Magufuli kwa kutufanyia Mambo makubwa katika nchi hivyo ni muhimu Watu wamuelezee na historia yake iwekwe katika mwandishi Watu wasome na vizazi vyao
Mavunde.

Hata hivyo amewataka wananchi kuwa wastamilivu juu ya Rais Magufuli na kumuombea maisha marefu ili aweze kutimiza ndoto zake huku akiwataka watanzania kutembea kifua mbele kujivunia kiongozi huyo kwani hata mataifa ya nje wanatamani kuwa na kiongozi wa aina hiyo.

Kwa upande wake Mwandishi wa Kitabu hicho Mathias Kabadi amesema kilicho msukuma kuandika Kitabu hicho ni pamoja na maisha ya unyonge nyakati za nyuma ,uzalendo wake na amekuwa Rais wa wanyonge.

Kabadi Amesema Magufuli ni zawadi ya watanzania na ni kielelezo tosha kuwa ni kiongozi bora na katika utawala wake ni mtatuzi wa watanzania.

Kingine kilichonisukuma kuandika historia ya Rais wetu amekuwa kiongozi wa vitendo ahadi zake zote alizoahidi alipokuwa anaingia madrakani mwaka 2015 ameyaishi na Kila mtu anamuona
 Mwandishi wa Kitabu hicho Kabadi.

Post a Comment

0 Comments