SERIKALI YATANGAZA BEI ELEKEZI YA MBOLEA


📌NA HAMIDA RAMADHANI

SERIKALI imetangaza bei elekezi ya mbolea ya kupandia (DAP) na kukuzia(Urea) kwa msimu wa mwaka 2020/21 nchi nzima kwa wastani wa shilingi 1,316 kwa mfuko wa kilo 50 wa UREA ikilinganishwa na msimu wa 2019/20. 

Kwa upande wa DAP bei imepungua kwa wastani wa shilingi 2,860 kwa mfuko wa kilo 50 ikilinganishwa na msimu wa 2019/20.

Hayo yamesemawa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati akitoa bei elekezi  ya uuzwaji wa mbolea nchini.

''Na bei hii ingeshuka zaidi lakini kutokana na janga la ugonjwa wa Corona na kupanda ghafla kwa viwango vya ubadilishanaji fedha sekta nyingi ziliathirika,''amesema.

Aidha, ameagiza viongozi wa mikoa kuhakikisha mbolea inafika kwa wakati kwa wakulima huku vyama vya ushirika vikitakiwa kuagiza kwa pamoja.


Ameeleza kwa upande wa DAP bei imepungua kwa wastani wa shilingi 2,860 kwa mfuko wa kilo 50 ikilinganishwa na msimu wa 2019/20.
h
Amefafanua pamoja na punguzo hilo la bei ya mbolea kwa msimu wa 2020/21 ukilinganisha na msimu wa 2019/20, vyama vya ushirika vilivyoshiriki zabuni ya BPS kwa msimu huu wa 2020/21 vitawauzia mbolea wanachama wao kwa bei nafuu zaidi ya bei elekezi inayotolewa na Serikali, hii ni kutokana na kwamba bei yao haijumuishi faida kama wanavyofanya wafanyabiashara.

Faida nyingine ni kwamba, mbolea iliyoagizwa na vyama vya ushirika imewafikia wanachama wao mpaka vijijini walipo.
Japhet Hasunga

Aidha, alisema wastani wa bei ya mbolea ya DAP kitaifa kuanzia leo kwa msimu wa 2020/21 itakuwa shilingi 55,573 kwa mfuko wa kilo 50 ikilinganishwa na shilingi 58,433 kwa mfuko wa kilo 50 msimu wa 2019/20.

Kwa upande wa mbolea ya UREA, wastani wa bei kitaifa kwa msimu wa 2020/21 itakuwa shilingi 48,070 kwa mfuko wa kilo 50 ikilinganishwa na shilingi 49,386 msimu wa 2019/20.

Amebainisha kuwa mchanganuo wa bei elekezi za mbolea ya DAP na UREA kwa Mkoa mmoja na mwingine zinatofautiana kutokana na umbali kutoka Dar es Salaam, hali ya barabara na gharama za usafiri.

Akizungumzia ulinganifu wa bei elekezi za msimu wa kilimo 2019/20 na 2020/21 kwa mfuko wa mbolea ya DAP kilo 50 kimkoa amesema Arusha ni 55,356 (2020/21) ikilinganishwa na 58208(2019/20), Dodoma 53925(2020/21) ikilinganishwa na 56790(2019/20).

Amesema Bei elekezi kwa mbolea zilizoingizwa na vyama vya ushirika kwa msimu wa 2020/21 zitakuwa shilingi 50,000 kwa mfuko wa kilo 50 wa DAP na shilingi 43,500 kwa mfuko wa kilo 50 wa mbolea aina ya UREA.

“Mwenendo wa bei elekezi za mbolea Namna COVID 19 itakavyoathiri bei za mbolea nchini Pamoja na kushuka kwa bei za mbolea kunakotegemewa katika msimu huu alisema pamekuwepo na changamoto ya kupanda ghafla kwa viwango vya ubadilishanaji fedha .

Hii ni kutokana na kuathirika kwa biashara za kimataifa (utalii, madini n.k.) kulikotana na ndege kuzuiwa kuruka kama njia mojawapo ya njia za kujikinga na janga la ugonjwa wa Corona ulioikumba Dunia tangu mwaka 2019 (COVID 19),”amesema Hasunga .

Alifafanua kuwa siku ya kutangaza zabuni ya kuingiza mbolea aina ya DAP Juni 11, 2020, viwango vya ubadilishaji fedha vilikuwa wastani wa Tshs 2,339 kwa US$.

“Hili ni ongezeko la 1.2% ikilinganishwa na viwango vya ubadilishaji fedha vya Tshs 2,311 kwa US$ 1 vilivyokuwepo katika zabuni za BPS zilizofunguliwa Novemba 25, 2019. Wakati mbolea za BPS zinaanza kuwasili nchini Julai 26, 2020 tayari viwango hivyo vilikuwa vimefumuka hadi kufikia sh 2,349 hadi 2,360 kwa US$ 1.

Hali hii si ya kawaida kwani kwa miaka iliyopita mfumuko haukuwa mkubwa kiasi hicho. Kutokana na mfumuko huo, punguzo la bei litakalotangazwa halitakuwa kubwa kama ambavyo ingetokea kama viwango vya ubadilishanaji fedha vingekuwa si vikubwa,”ameeleza Hasunga.

Post a Comment

0 Comments