SHAMSIA GROUP YAIMIZA JAMII KUWAKUMBUKA WAGONJWA HOSPITALINI



📌NA HAMIDA RAMADHANI

MWENYEKITI wa Shamsia Group Weman and Children Ogarnazation Tunu Dachi amesema kuwa wagonjwa hospitalini ni sehemu ya watu waliosahaulika hasa katika nyakati muhimu kama  za sikukuu.

Ameeleza hayo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na CPC blog mara baada ya kutoa mkono wa huruma na kulisha chakula cha mchana kwa wagonjwa na wauguzi wote katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General).

Amesema Shamsia Group imekuwa na utamaduni wa kutoa chakula kwa wagonjwa Kila mwaka Mara baada ya Eid Al Hajji mfungo Tatu na mwaka huu ni mwaka wa saba(7) kufanya zoezi hilo.

Tuseme wazi Wagonjwa ni Watu waliosahaulika hivyo niiombe jamii na wadau mabalimbali tuguswe na matatizo ya watu na tujitoe kuwasaidia Wagonjwa kwani suala la ugonjwa ni la kila mmoja
Tunu Dachi

Hata hivyo ameziomba Taasisi zingine ziguswe kwa wakati wao kuja kutoa mkuno wa faraja  kwa wagonjwa hawa ilinawao ni wajione Watu katika jamii.

Post a Comment

0 Comments