TMDA,TIC NA TRA ZAPONGEZWA KWA KUWA MSTARI WA MBELE KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI.

Naibu waziri Viwanda na biashara Eng.Stella Manyanya akipata maelezo mafupi kutoka kwa kaimu Meneja TMDA Sonia  Mkumbwa Viwanja vya nanenane Nzuguni jijini Dodoma


📌NA FAUSTINE GIMU

Naibu Waziri wa viwanda na biashara mhandisi Stella Manyanya amezipongeza mamlaka ya Dawa na vifaa tiba[TMDA] kituo cha uwekezaji Tanzania [TIC] pamoja na Mamlaka ya mapato Tanzania[TRA]kwa kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwemo kutoa elimu kupitia  vyombo vya habari hali ambayo imekuwa njia nyepesi ya kuwafikishia elimu wananchi kwa haraka zaidi.

Akizungumza Agosti,6,2020 alipotembelea mabanda ya maonesho katika banda la  mamlaka ya dawa na vifaa tiba [TMDA]banda la kituo cha uwekezaji  Tanzania[TIC] Pamoja na Mamlaka ya mapato Tanzania [TRA]Mhandisi Manyanya amesema taasisi hizo  zimekuwa mstari wa mbele katika kuwafikishia ujumbe wananchi hususan vijijini hivyo amezitaka taasisi hizo kuendelea kuwa na juhudi zaidi katika kuwaelimisha Watanzania .

“Kwa kweli niseme kati ya taasisi ambazo zinajitangaza vizuri katika vyombo vya habari ni TMDA  na TIC kwa kweli nawapongeza sana kwa sababu bila kutoa elimu kwa umma huwezi kuwasaidia hawa wananchi,huwezi kusubiri nanenane tu ndipo utoe elimu  ,TMDA  mnajitahidi sana  , Pia TIC Mnafanya vizuri ndio maana watanzania wazawa sasa wanachangamkia fursa za uwekezaji  dhana ya kuwa mwekezaji lazima awe mzungu sasa haipo,TRA nanyi mpo vizuri ndio maana makusanyo yameongezeka maradufu   hii inatokana na wananchi kuelewa umuhimu wa kodi kwa mandeleo ya nchi“amesema.

Afisa elimu kwa umma TMDA kanda ya kati Hussein Makame akitoa
elimu kwa wateja waliotembelea banda hilo


Aidha,Mhandisi Manyanya amesema kuna haja sasa Mamlaka ya mapato Tanzania [TRA]kuwa na mpango wa kutangaza zawadi kwa walipaji kodi vizuri  ili kuleta hamasa zaidi katika ulipaji wa kodi ili kuongeza pato la taifa.

Kaimu meneja wa TMDA kanda ya kati Sonia Mkumbwa amesema wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi ikiwemo kuwaelimisha juu ya kukagua dawa kabla ya kununua huku mwakilishi wa TIC kanda ya kati Abubakary Ndatwa akisema kituo cha Uwekezaji  Tanzania kimekuwa kikitoa miongozo mbalimbali  katika suala zima la uwekezaji ikiwa ni pamoja na taratibu za umilikaji ardhi kwa kufuata sheria .

Post a Comment

0 Comments