."TUTAWASHUGHULIKIA WOTE WATAKAOHATARISHA AMANI DODOMA"-RPC MUROTO


📌NA.FAUSTINE GIMU GALAFONI
Jeshi la polisi Mkoani Dodoma limesema limejipanga kwa mashambulizi kwa wale wote watakaokuwa na nia ovu ya kufanya vurugu na kuhatarisha amani katika kampeni  za vyama mbalimbali za siasa.
Akizungumza na waandishi wa jijini Dodoma Kamanda wa polisi  mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amebainisha kuwa makundi yote ya ovyo ambayo yamejiandaa kwa ajili ya  kuleta vurugu yatashughulikiwa na kazi ya jeshi la polisi ni kulinda amani ya Tanzania.
Tanzania huwa naifananisha na mto wa maji mtulivu,mara nyingi  huwezi ukaona kwa macho umetulia ndani ya mto huo kuna viumbe  maisha yao  yanategemea hapo, hivyo hakuna mnyama anayekubali kuchezewa hayo maji kenge wataenda sehemu zao na mamba sehemu zao ikimaanisha kuwa jeshi la polisi halitakaa kimya amani ya Tanzania ichezewe 
Aidha,Kamanda Muroto amesema kuwa jeshi la Polisi litahakikisha linafuatilia kwa makini mwenendo wa kampeni na kubainisha kuwa Tanzania haina Mjomba wala shangazi nje ya nchi  huku akiwataka waandishi wa Habari kutumia kalamu zao vizuri kuhakikisha hakuna Habari za uchochezi.
“Tanzania haina mjomba wala shangazi nje nchi nyingi ambazo zinatuzunguka zimekuwa zikija hapa kwa sababu zimekuwa zikipata matatizo kwa hiyo sisi kama jeshi la polisi tunahakikisha tunalinda amani na waandishi wa Habari muwe sehemu ya Watanzania kuhakikisha hali ya amani na utulivu inakuwepo”amesema.


Post a Comment

0 Comments