UWT WAPO TAYARI 'KULIAMSHA DUDE'



📌NA DEVOTHA SONGORWA

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania, mkoa wa Dodoma, Neema Majule amesema kuwa maandalizi kuelekea uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu yamefikia hatua nzuri.

Mwenyekiti huyo amesema kwamba uamuzi wa kufanyika uzinduzi August 29 katika makao makuu ya nchi ni heshima kubwa na itatoa picha halisi namna Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilivyojipanga kushiriki katika uchaguzi kikamilifu.

Uzinduzi huo utafanyika tarehe 29 mwezi huu kutwa katika Uwanja wa Jamhuri mgeni rasmi akiwa ni Rais, Dk.John Magufuli.

Amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura kama haki yao kikatiba akisema ni wakati wao sasa kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi atakayekuwa tayari kutetea haki za wanawake na kumfanya mwanamke kutambua ana sehemu ya kufanya kufikia kilele cha mafanikio.

Maandalizi yanaendelea vizuri usafi wa uwanja umefanyika, kutakuwa na wawakilishi kutoka mikoani na unajua huu ni uzinduzi wa kampeni kitaifa, wasanii watakuwepo tumejipanga vizuri sana na vikundi vya hamasa na wanachama wenyewe watakuwepo mambo yamepamba moto
Neema Majule.

Pia Neema ameeleza kwamba wakati wote wa kampeni wagombea wamejiandaa kufanya kampeni kwa kuzingatia sheria kwa kunadi sera zao na ahadi zao wa wapiga kura huku akisema kwamba katika hili vijana hawajaachwa nyuma kwani wana mchango mkubwa katika Taifa lolote lile hivyo ni wakati wao sasa kuunga mkono chama kwa kuhakikisha CCM inapata ushindi wa kishindo.

Katika hatua nyingine aliwataka wagombea hasa wanawake waliojitokeza kuchukua fomu lakini hawakufanikiwa kuingia katika kinyang'anyiro kutokata tamaa kwani wameonyesha uthubutu wa hali ya juu hivyo watumie mwanya huyo kuwapa kura waliochaguliwa kumuwezesha mgombea wa kiti cha Urais Ndugu John Pombe Magufuli kushika tena miaka mitano kuhudumia watanzania.

Tumefanya kikao cha ndani tukawaita wagombea wote iwe alipita au hakupita karibu wagombea 400 wanawake sasa wameamua na ni jeshi kubwa tumewaomba waende wakahamasishe wanawake wengine kukipigia kura ya ndiyo Chama Cha CCM nafasi zote Rais, Wabunge na Madiwani wanawake tunaweza
Neema Majule.

Akizungumzia makundi maalumu Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba CCM ni Chama ambacho kinakumbatia makundi maalumu yote bila ubaguzi na kimekuwa kikitoa nafadi za uongozi hata kwa watu wenye ulemavu akisema wana haki kisheria kama watu wengine kwani ulemavu wao hauzuii haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa ni kazi kwao kuamini kwamba wana uwezo mkubwa kufanya mageuzi ya kimaendeleo.

Yaani katika kundi ambalo Chama hiki kinawaangalia kwa jicho la tatu ni watu wenye ulemavu tumeshuhudia Rais wa Awamu ya Tano, Dk.John Magufuli alianzisha asilimia 10 kutoka kila Halmashauri kutoa asilimia 2% kwa wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi kwanini tusimpigie tena kura ya ndiyo mtetezi wa wanyonge.
Neema Majule

Aidha kuhusu vitendo vya rushwa katika zoezi la uchaguzi amesema kwamba hakuna haki katika rushwa na CCM ni Chama amacho kinafuata misingi ya sheria na kipo mstari wa mbele kupiga vita rushwa huku akiwataka wapiga kura nao kutowafumbia macho wagombea wasiowaminifu.

Post a Comment

0 Comments