WAKULIMA, WASINDIKAJI TUMIENI LUGHA YA KISWAHILI KUTAMBULISHA BIDHAA


📌NA HAMIDA RAMADHANI 

NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara mhandisi Stella Manyanya amewaka Wakulima na wasindikaji wa vyakula kutumia Lugha ya kiswahili sanifu katika kutambulisha bidhaa zao walizofungasha ili kumsaidia mtanzania kujua bidhaa anayotumia.

Aliongea hayo Leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wakulima na watafiti katika Banda  la Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania (TARI).

Tunatakiwa tuwe na utaratibu wa kutambulisha bidhaa zetu kwa Lugha yetu ya kiswahili lugha ambayo inaeleweka kwa kila mtu, tuache tabia ya kutamburisha bidhaa zetu kwa lugha za kigeni  kingereza
Mhandisi Manyanya 

Na kuongeza kusema "Sasa kutokana na hayo napenda kutoa Rai kwa wakulima wote kutambua kwamba maonyesho mengine  2021 bidhaa zote zilizofunashwa na kuandikwa kwa Lugha ya kingereza hazitaingia kwenye maonyesho hayo ,"Amesema Naibu Waziri huyo Manyanya.

Hata hivyo amesema serikali imekuwa ikisisitiza wakulima na wachakataji wa vyakula kutumia Lugha laisi kwenye  bidhaa zao lakini jambo hilo limeshindwa kutekelezeka.

Kaulimbiu ya Maonesho ya Wakulima na Wafugaji ya mwaka 2020  inasema kwamaendeleo ya Kilimo,Ufugaji na Uvuvi chagua kiongozi bora

Post a Comment

0 Comments