WANAWAKE ,VIJANA WAASWA KUTUMIA UONGOZI KWA MASLAHI YA TAIFA



📌NA FAUSTINE GIMU GALAFONE 
CHAMA cha wanasheria wanawake Tanzania (TAWLA),kwa kushirikiana na Taasisi ya vijana TYC,pamoja na WE EFFECT,wamezindua  mradi wa  miaka mitatu (3) wa kuongezea Uwezo  kwa ushiriki wa wanawake na vijana katika masuala ya uongozi
Akizungumza katika uzinduzi huo, uliofanyika leo Jijini Dodoma Mgeni rasmi ambaye ni Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini {NGO} kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,Bi Vickness Mayao  ametoa wito  kwa Wanawake na vijana ambao watachaguliwa katika nafasi za uongozi kutumia nafasi watakazopata kwa maslahi ya Taifa.
Aidha amewataka  kuzingatia kanuni na maadili ya uchaguzi kulingana na Sheria za uchaguzi huku akiwataka TAWLA kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii kuhusu vijana na wanawake kuongeza ushiriki wa nafasi mbalimbali za uongozi.
Kwa upande wake Mkurugenzi  Mkuu wa TAWLA,Tike Mwambile akielezea lengo la mradi huo amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuweza kuongeza usawa wa kijinsia katika  ushiriki wa uchaguzi kwa wanawake na vijana.
Nao washiriki wa mradi huo toka katika Mikoa ya Arusha na Tanga wametoa maoni yao.
mradi huo ambao unaanza kutekelezwa mwaka huu wa 2020  hadi 2023 unafanyika katika mikoa mitatu ya Arusha,Tanga na Mwanza.

Post a Comment

0 Comments